Pata taarifa kuu
Tanzania-Usalama

Tanzania : shambulio la bomu latikisha mji wa kitalii wa Arusha

Watu wanane wamejeruhiwa na mwengine mmoja akiwa mahututi katika shambulio la bomu dhidi ya mgahawa uliyoko katika mji wa kitalii wa Arusha, kaskazini mwa Tanzania, polisi imethibitisha.

Mji wa Arusha
Mji wa Arusha Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

“Hakuna maafa yaliyotokea, lakini watu wanane ndio wamejeruhiwa, huku mmoa akiwa katika mahututi”, amesema Issaya Mngulu, afisa wa juu wa polisi ya Tanzania, huku akibaini kwamba majeruhi wote ni raia wa Tanzania.

Mngulu ameseama kwamba bomu hilo lilirushwa kupitia dirishani. Lakini mpaka sasa polisi haijafahamisha kuhusu chanzo cha mlipuko huo, uliyotokea jumatatu jhii jioni.

Shambulio hilo lililenga mgahawa unaomilikiwa na raia wa India, ambao unapatikana katika mtaa muhimu wa mji wa Arusha, ambao unatembelewa na raia werngi wa kigeni na viongozi tawala wa eneo hilo.

Damu zimekua zimetapakaa kwenye meza na viti , huku gilasi zikivunjwa, ameshuhudia mwandishi wa shirika la habari la AFP.

Arusha ni mji wa kitalii nchini Tanzania, ambao unachangia kwa kiasi kikubwa kuingiza mapato katika sekta ya uchumi.

Watuhumiwa wawili ambao ni raia wa Tanzania wamekamatwa, amesema kiongozi wa polisi , biala hata hivo kutoa taarifa zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.