Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-Mgomo

Afrika Kusini : wafanyakazi kutoka viwanda vya chuma waaendelea na mgomo

Shirikisho la wafanyakazi kutoka viwanda vya chuma na wahandisi nchini Afrika ya kusini limearifu hii leo kuwa mgomo wao uliodumu kwa majuma mawili sasa utaendelea mpaka muajiri wao atakapotimiza matakwa yao.

Mgomo wa wawafanyakazi kutoka viwanda vya vyuma unaendelea Afrika Kusini.
Mgomo wa wawafanyakazi kutoka viwanda vya vyuma unaendelea Afrika Kusini. REUTERS/Skyler Reid
Matangazo ya kibiashara

Takribani wafanyakazi laki 2 kutoka viwanda hivyo vya chuma waliingia katika mgomo mwanzoni mwa mwezi huu Julai wakidai nyongeza ya mshahara.

Hii

Katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi wa vyuma nchini Afrika Kusini, Numsa,  Irvin Jim
Katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi wa vyuma nchini Afrika Kusini, Numsa, Irvin Jim Reuters

leo Irvin Jim, katibu mkuu wa shirikisho la wafanyikazi wa viwanda vya chuma wafanyakazi hao wamekataa hoja iliyotolewa na waajiri kwa kutokamilika vigezo vyao.

Bwana Jim alisema wafanyakazi hao watakubali mkataba wa mwaka mmoja au mitatu kwa asilimia 10 kwa kila mwaka na kulipia makazi kinyume na hao mgomo utaendelea na kuhusisha sekta nyingine.

Chama cha wafanyakazi kutoka viwanda vya chuma Numsa kimekataa mapendekezo ya muajiri wake, huku kikibaini kwamba kitaendelea na mgomo uliyoanza Juali 2 katika sekta ya chuma na ujenzi.

“Tunataka tufahamike vizuri: mgomo unaendelea, na tunatolea wito wadau wetu wote kuendelea na mgomo, huku tukiwahimiza wafanayakazi wengine katika sekta mbalimbali”, amesema katibu mkuu wa Numsa, Irvin Jim katika mkutano na waandishi wa habari.

Numsa imebaini kwamba imewahimiza wafanyakazi 220.000 kutoka viwanda na mashirika 10.000 kwa kuitikiya mgomo, ambao umesababisha shughuli kuzorota katika makampuni binafsi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.