Pata taarifa kuu
DRC-UPINZANI-Sheria-Siasa

DRC : upinzani wataka rais Kabila afunguliwe mashtaka

Upinzani nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umemuomba rais wa marekani Barack Obama, jumuiya ya kimataifa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kumfungulia mashtaka Rais Joseph Kabila kwenye mahakama ya ICC mjini The hague, Uholanzi.

Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Etienne Tshisekedi (kushoto) et Vital Kamerhé (kulia), viongozi wawili wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Etienne Tshisekedi (kushoto) et Vital Kamerhé (kulia), viongozi wawili wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. AFP/ Montage RFI

Katika waraka uliotumwa kwa Rais wa Marekani na Jumuiya ya kimataifa, Umoja huo wa vyama vya kisiasa ikiwa ni pamoja na chama cha UDPS cha Etienne Tshisekedi wa Mulumba na chama cha UNC cha Vital Kamerhe pamoja na vyama vingine vimemtuhumu rais Kabila kuwa chanzo cha mauwaji na unyanyasaji nchini DRC.

Miongoni mwa uhalifu unaobainishwa na umoja huo, ni pamoja na mauaji ya waandishi wa habari na wanaharakati wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na mwenyekiti wa shirika la kutetea haki za binadamu la “La Voix des Sans Voix” ama sauti ya watu wasio na sauti, Floribert Chebeya.

Aidha, muungano huo umesisitiza kuwa rais Joseph Kabila anapaswa awajibishwe kwa kushindwa kupiga vita rushwa, uporaji wa maliasili, kwa ukandamizaji dhidi ya wafuasi wa Bundudia Kongo, mauaji ya vijana wa Kuluna na kutoweka kwa maafisa kadhaa kutoka jimbo la Equateur.

Ombi hilo la upinzani pia linamtaka rais Kabila kutengwa kidiplomasia kwa tuhuma hizo ambazo hadi sasa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo haijazungumzia bado.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.