Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-JIHADI-Usalama

Raia wa Afrika Kusini wasadikiwa kujiunga na makundi ya wanajihadi

Serikali ya Afrika Kusini imeeleza wasiwasi wake kufwatia taarifa zilizochapishwa hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwa baadhi ya raia wa nchi hiyo miongoni mwa wanajihadi wanaoendesha mashambulizi nchini Syria na Iraq.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ambaye serikali yake inatiwa wasiwasi na madai ya raia wa Afrika kusini kujiunga na makundi ya wanajihadi..
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ambaye serikali yake inatiwa wasiwasi na madai ya raia wa Afrika kusini kujiunga na makundi ya wanajihadi.. REUTERS/Sumaya Hisham/Pool
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya mambo ya nje nchini humo imeanzisha uchunguzi kubaini kuwa mtu aliyejitambulisha katika video kwenye mtandao wa Youtube kuwa ni Abu al-Ab Shui ni raia wa Afrika kusini, ambaye anaendesha kampeni ya kuwataka raia wa nchi hiyo kujiunga na wapiganaji wa Kiislam nchini Syria na Iraq.

Katika video hiyo, kundi la watu linaonekana likiadhimisha sherehe za Eid el Fitr mwishoni mwa mwezi wa Ramadhan katika mji mkubwa, akiwemo kati yao mtu huyo ambaye amedai kuwa raia wa Afrika Kusini akiwa na mtoto mikononi mwake.

Miezi michache iliyopita, nchi ya Afrika Kusini ilieleza wasiwasi wake kuhusu uwezekano wa kuwepo nchini humo kwa wanamgambo wa nchi ya Nigeria wa Boko Haram kusajili vijana katika nchi hiyo ambayo kwa takwimu za hivi karibuni idadi ya waislamu inafikia laki saba na hamsini elfu.

Wataalam ambao wameona video hiyo wanatilia mashaka kuhusu uhalisia wa madai ya mtu huyo kufwatia lafudhi yake, lakini mashirika mbalimbali ya kiislam Afrika Kusini yameonya kuwa tayari kumekuwepo na majaribio ya kundi hilo kuwasajili vijana nchini humo, hasa katika maeneo ya Durban na Cape Town.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.