Makundi ya kislamu yaaendelea kujidhatiti
Wakati jeshi nchini Nigeria likiongeza mashambulizi zaidi kukabilia na wapiganaji wa kiislamu wa Boko Haram ambao wameendelea kuhatarisha usalama nchini humo, ripoti mpya zinaonesha kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la makundi ya kiislamu kwenye ukanda wa mashariki ya kati hadi Asia.
Imechapishwa:
Cheza - 01:49
Ripoti hiyo inasema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la makundi haya ya kiislamu kayika kipindi cha miezi 12 iliyopita kutokana na vita nchini Syria na mashambulizi ya Boko Haram nchini Nigeria, shirika la kimataifa la utafiti la Pew limesema kwenye ripoti yake.
Ripoti hii inasema kuwa makundi ya Al-Qaeda, Hezbollah, Boko Haram na hata kundi la Hamas ambalo limeshinda hata kwenye uchaguzi wa Palestina yameanza kupoteza uungwaji mkono na makundi haya.
Wachambuzi wa masuala ya usalama na siasa wanasenasema makundi haya ya kislamu yanaonekana kuwa yanafadhiliwa kimataifa na kundi la Al Qaeda, huku wakibaini kwamba makundi hayo huenda yana mafungamano na kundi hilo la Al Qaeda.