Pata taarifa kuu

Blinken: Marekani 'imeamua' kupata makubaliano ya Israel na Hamas 'sasa'

Marekani "imedhamiria" kwamba Israel na Hamas wahitimishe makubaliano ya kusitisha mapigano "sasa", yanayohusiana na kuachiliwa kwa mateka, ametangaza leo Jumatano Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, akizuru Israel.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken na Rais wa Israel Isaac Herzog mjini Munich Februari 17, 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken na Rais wa Israel Isaac Herzog mjini Munich Februari 17, 2024. AFP - THOMAS KIENZLE
Matangazo ya kibiashara

"Hata katika nyakati hizi ngumu, tumedhamiria kupata usitishaji wa mapigano kuwarudisha mateka nyumbani na kufanikisha sasa. Na sababu pekee kwa ya kutotekelezwa kwa mkataba huo ni Hamas,” Blinken amesema mjini Tel Aviv, akikutana na Rais wa Israel Isaac Herzog.

Wakati huo huo Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu Martin Griffiths ameonya kwamba licha ya wito wa kimataifa kwa Israel kuiokoa Rafah katika Ukanda wa Gaza, "operesheni ya ardhini iko karibu". Amesema operesheni hiyo itakuwa "janga lisiloweza kuelezeka."

Nalojeshi la Marekani linatazamiwa kukamilisha ujenzi wa gati ya muda katika pwani ya Gaza siku ya Alhamisi ili kuruhusu misaada zaidi ya kibinadamu kuwasilishwa katika eneo la Palestina lililozingirwa, rais wa Cyprus alitangaza siku ya Jumanne.

Nchi wapatanishi wakati huo huo zinasubiri jibu kutoka kwa Hamas kwa pendekezo la usitishaji vita wa siku 40 unaohusishwa na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa katika Ukanda wa Gaza. Kwa upande wake, Israel itasubiri "hadi Jumatano jioni" kwa jibu kutoka kwa Hamas kuhusu pendekezo la kusitisha vita linalojadiliwa mjini Cairo kabla ya kufanya uamuzi wa kutuma ujumbe huko, afisa wa Israel ameliambiashirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.