Abbas aitaka Marekani kushawishi Israel kutothubutu kushambulia Rafah
Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas, ameitaka Marekani kusaidia, kwa kuizuia mpango wa jeshi la Israeli kuvamia mji wa Rafah kwa kutuma vikosi vyake vya ardhini.
Imechapishwa:
Kiongozi huyo wa Palestina amesema iwapo Israel itavamia mji wa Rafah, itakuwa ni janga kubwa sana kwenye historia ya raia wa Palestina, na Marekani ndio nchi pekee yenye uwezo wa kuzuia mpango huo wa mshirika wake Israeli.
Aidha, rais Abbas amesema anahofia kuwa wanajeshi wa Israeli wanapanga kuushambulia ukingo wa Magharibi, baada ya kumalizana na ukanda wa Gaza.
Katika hatua nyingine, Saudi Arabia inasema inataka uthabiti wa kikanda ikionya kuwa, vita vinavyoendelea kati ya Israeli na Hamas, ikisema inaharibu mshikamo wa nchi za kikanda.
Wakati hayo yakijiri, kiongozi wa juu wa kundi la Hamas Khalil al-Hayya amesema, kundi hilo litajibu mapendekezo ya Israeli kuhusu mpango wa kusitisha vita kwenye ukanda wa Gaza watakapokutana siku ya Jumatatu nchini Misri.