Pata taarifa kuu

Misri inatoa wito kwa Hamas na Israel kujizuia kwa ajili ya kusitisha mapigano Gaza

Misri inatoa wito kwa Hamas na Israel "kujizuia" ili kufikia "haraka iwezekanavyo" suluhu katika mapigano huko Gaza pamoja na kuachiliwa kwa mateka, kulingana na taarifa kutoka kwa Wizara yake ya Mambo ya Nje.

Wakaazi wa al-Mawasi watoroka mji huo na kukimbilia eneo salama zaidi huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Mei 9, 2024.
Wakaazi wa al-Mawasi watoroka mji huo na kukimbilia eneo salama zaidi huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Mei 9, 2024. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Choukri amesisitiza "umuhimu wa kuzitaka pande husika kujizuia na kupeleka juhudi zote zinazohitajika ili kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na hivyo kukomesha janga la kibinadamu" Gaza, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imesema.

Hayo yanajiri wakati Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant amewaambia "maadui na marafiki" wa taifa lake kwamba watafanya kinachostahili kufikia malengo ya vita Gaza, ikiwa ni jibu kwa Marekani iliyotaka isitishe operesheni huko Rafah.

Kauli hiyo aliyoitoa katika hafla ya kuwakumbuka waliouwawa katika vita vya Israel, inafuatia onyo la Rais Joe Biden, akisema kwamba Marekani itasitisha utoaji wa silaha kwa Israel kama taifa hilo litaendelea na mashambulizi yake katika eneo la Rafah, eneo ambalo zaidi ya Wapalestina milioni moja walioachwa bila ya makazi, wanajipatia hifadhi.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na ofisi yake, Waziri Gallant amesema wataendelea kuwa madhubuti, watafanikisha malengo yao, watayashambulia makundi ya Hamas na Hezbollah na kufanikisha lengo la kiusalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.