Pata taarifa kuu

Gaza: Hamas yatangaza kukubali kusitisha mapigano kutoka kwa wapatanishi wa Misri na Qatar

Kundi la Hamas ilimetangaza siku ya Jumatatu, Mei 6, 2024, kwamba limekubali pendekezo la kusitisha mapigano lililotolewa na wapatanishi, Misri na Qatar, kwa Ukanda wa Gaza. Afisa wa Israel anasema pendekezo la kusitisha mapigano lililoidhinishwa na Hamas halikubaliki kwa Israel, linaripoti shirika la habari la REUTERS.

Watu waliokimbia makazi yao huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, tarehe 6 Mei 2024.
Watu waliokimbia makazi yao huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, tarehe 6 Mei 2024. © REUTERS - Hatem Khaled
Matangazo ya kibiashara

Ismail Haniyeh, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, alizungumza kwa simu na Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdelrahmane Al Thani na Waziri wa Ujasusi wa Misri Abbas Kamel na kuwafahamisha kwamba Hamas imeidhinisha pendekezo lao la "makubaliano ya kusitisha mapigano," kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya HAmas.

Afisa wa Hamas ametangaza, kwa sharti la kutotajwa jina, kwamba "mpira sasa uko katika kambi " ya Israel, ambayo ina chaguo "kati ya kukubali makubaliano ya kusitisha mapigano na kuyazuia."

Maelezo ya pendekezo la hivi punde lililotolewa na wapatanishi bado hayajajulikana.

Tangazo kwamba Hamas imekubali pendekezo la kusitisha mapigano limepokelewa kwa matukio ya shangwe na milio ya risasi angani huko Rafah, mji ulioko kusini mwa Ukanda wa Gaza uliozingirwa ambapo Israel inapanga kufanya mashambulizi makubwa ya kijeshi.

Watu wanashangilia na kumtukuza Mungu, anaripoti mwandishi wa shirik la habari la AFP, aliyeko katika eneo hilo, “watu wanalia kwa shangwe na risasi zinarushwa hewani katika kusherehekea.”

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.