Pata taarifa kuu
BURUNDI-Siasa-Haki za binadamu

Burundi: Maiti zaonekana kwenye ziwa Rweru

Habari inayogonga vichwa vya habari na ambayo imekua gumzo nchini Burundi ya maiti ambazo zinaendelea kuonekana katika ziwa Rweru kaskazini mashariki mwa taifa hilo, kwenye mpaka na Rwanda.

Ramani ya Burundi
Ramani ya Burundi RFI
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya miili 10 ikiwa ni pamoja na wanaume, wanawake na vijana imeonekana ikielea kwenye ziwa Rweru tangu jumamosi Agosti 23 mwaka 2014, huku baadhi ya miili hiyo ikifungwa kamba.

Wavuvi katika ziwa la Rweru, wamebaini kwamba tangu mwezi Julai wamekua wakiona kati ya maiti sita na arobaini zikielea kwenye maji ya ziwa hilo, linalopatikana kaskazini mashariki mwa Burundi. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kibinafsi mjini Bujumbura, ni wiki moja sasa tangu watu wapige kelele kuhusu hali hiyo.

Akihojiwa na idhaa ya kifaransa ya RFI, jana jumapili, mwakilishi wa wavuvi katika wilaya ya Giteranyi iliyokaribu na ziwa Rweru, amethibitisha kwamba alijielekeza pamoja na wanajeshi wa majini karibu na mto Kagera ambako ziwa hilo linamwaga, wakakuta maiti mbili, ambayo moja ilikua ikifungwa ndani ya mfuko.

“Hatungeweza kuzisitiri maiti hizo kwani zilikua zimeharibika “, amesma mwakilishi huyo, huku akibaini kwamba waliamua kuachia maiti hizo ndani ya maji, kama walivyofanya wavuvi wengine miezi iliyopita.

Maiti hizo zimesababisha hali ya taharuki nchini Burundi, ambapo watu bado wana kumbukumbu ya wafuasi wa vyama vya upinzani waliyouawa na kutupwa katika mto Ruvubu (mashariki) na mto Rusizi (magharibi), tangu mwaka wa 2006.

Hata hivo, kiongozi wa mkoa wa Muyinga, Manirabarusha Carine, akihojiwa na idhaa ya kifaransa ya RFI, ameapa akisisitiza kwamba miili hiyo ya watu inayoendelea kuonekana katika ziwa Bweru sio raia wa mkoa wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.