Pata taarifa kuu
BURUNDI

Upinzani nchini Burundi waeleza wasiwasi wa kuzuka vurugu za uchaguzi mwaka ujao

Mwanaharakati wa upinzani nchini Burundi Jean-Claude Bikorimana ameelezea wasiwasi wa kuzuka kwa uchaguzi wa vurugu nchini humo baada ya kushambuliwa na tawi la vijana wa chama tawala na kumjeruhi kifuani.

Pierre-Claver Mbonimpa katika chumba cha mahakama Ijumaa, Julai 4, 2014, akisubiri kuanza kwa kesi yake
Pierre-Claver Mbonimpa katika chumba cha mahakama Ijumaa, Julai 4, 2014, akisubiri kuanza kwa kesi yake RFI/Esdras Ndikumana
Matangazo ya kibiashara

Bikorimana mkulima mwenye umri wa miaka 26 amesema kuwa yeye ni miongoni mwa wafuasi 50 wa chama cha Upinzani nchini Burundi cha Movement for Solidarity and Development (MSD) ambao walishambuliwa na Imbonerakure wapatao 150 wakiwa wamejihami kwa marungu na mawe wakati wakicheza mpira kwenye mji wa Gihanga mnamo Oktoba mwaka jana.

Upinzani na makundi ya haki za binadamu nchini Burundi wanasema ghasia za kisiasa zimekuwa zikiongezeka katika nchi hiyo ndogo ya Afrika ya kati ambayo iliondokana na vita ya miaka 13 ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2006,wakati huu inapoelekea katika uchaguzi wa rais mwaka Ujao.

Rais Pierre Nkurunziza kwa kiasi kikubwa anatarajiwa kugombea kwa muhula wa tatu na kupindisha mihula miwili ambayo inaruhusiwa na katiba ya taifa hilo.

Mwezi Machi, Mamlaka nchini Burundi zilipiga marufuku Mamlaka marufuku mbio za makundi ya watu wawili au zaidi kwa misingi kwamba vyama vya upinzani wanawatumia kuandaa ghasia.

Mwezi huu, mkuu wa shirika kuu la kutetea haki za binadamu nchini Burundi Pierre-Claver Mbonimpa alishitakiwa kwa “kuhatarisha usalama wa taifa” baada ya kueleza kuwa wafuasi wa Imbonerakure walikuwa wakipewa mafunzo ya kijeshi na silaha katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.