Pata taarifa kuu
RWANDA-RDF-Usalama

Maafisa wastaafu wa jeshi la Rwanda waendelea kukamatwa

Jeshi la Rwanda limetangaza kukamatwa kwa afisa wake mustaafu mwingine Kapteni David Kabuye anayetuhumiwa kwa uhalifu, amesema Jenerali Joseph Nzabamwita, msemaji wa jeshi hilo.

AFP PHOTO/ Tony KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Msemaji huyo wa jeshi amebaini kuwa uchunguzi bado unaendelea na kusisitiza kwenye vyombo vya habari kwamba taratibu za kisheria kumweka David Kabuye kizuwizini zimezingatiwa na kwamba familia yake wamepewa taarifa.

Juma lililopita, jeshi hilo limetangaza kuwekwa kizuwizini kwa Jenerali mstaafu Frank Rusagara kwa kumhusisha na vitendo vya uhalifu na kuanza kuzua maswali miongoni mwa wanyarwanda hasa waishio nje ya nchi, wakitabiri kuwa ifikapo mwaka 2017 maafisa wa jeshi zaidi watakamatwa kama alivyoandika David Himbara mshauri wa zamani wa rais Rais Paul Kagame kwenye akaunti yake ya facebook.

Wakuu kadhaa wa jeshi hilo wamekumbwa na chunguzi pamoja na tuhuma ambapo mkuu wa majeshi wa kwanza Kayumba Nyamwasa alipoteza nafasi yake mwaka 2002, huku mwaka 2010 maJeneral Karenzi Karake na Charles Muhire wakiwekwa kizuwizini kwa tuhuma za uzembe mkubwa kazini. Mwaka 2012 ilikuwa ni zamu ya maJeneral Ibingira, Rutatina, Gumisiriza na Kanali Dan Munyaza, waliotuhumiwa kutumia rasilimali ya Congo kinyume cha sheria.

Aidha, mwaka 2013, mkuu wa majeshi Charles Kayonga alipoteza nafasi yake, na baada ya miezi michache ya kutokuwa na shughuli ya aina yoyote aliteuliwa balozi wa Rwanda nchini China, huku Jeneral Ceaser Kayizari akiteuliwa balozi na Rwanda nchini Uturuki.

Hata hivo, habari ambazo bado hazijathibitishwa , zinabaini kwa huenda kuna maafisa wengine katika jeshi na serikali ya Kigali wanaofanyiwa uchunguzi ili wawekwe jela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.