Pata taarifa kuu
EBOLA-NIGER-AFYA

Ebola: Niger yakabiliana na mambukizi ya Ebola

Hata kama Niger haijaorodhesha visa vya Ebola haujaripotiwa serikali imechukua hatua za kukabiliana na ugonjwa huo.

Hatua kali za kupambana dhidi ya virusi vya Ebola zimechukuliwa katika mji wa Agadez, na maeneo mengine Niger.
Hatua kali za kupambana dhidi ya virusi vya Ebola zimechukuliwa katika mji wa Agadez, na maeneo mengine Niger. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Tangu mlipuko huo wa ugonjwa wa Ebola kuripotiwa katika nchi za magharibi mwa Afrika, viongozi wa afya nchini Niger walianzisha kampeni kubwa ya kuhamasisha raia, katika maeneo mbalimbali, hususan katika shule, kwa namna ya kukabiliana na mambukizi ya Ebola.

Shuleni, waalimu wamekua wakihamasisha wanafunzi jinsi ya kupambana na kuenea kwa virusi vya Ebola, na mkuna baaadhi ya shule ambazo zimeanzisha visomo vya kuhamasisha wanafunzi kwa namna ya kukabiliana na Ebola, hususan kuosha mikono kwa sabuni kila baada ya kutoka chooni.

Kwa mujibu wa mwalimu mmoja wa shule katika mji mkuu wa Niger, Niamey, visomo hivo vinatolewa kwa aina hiyo. “ kila mara wanapotoka chooni wanatakiwa kuosha mikono yao kwa sabuni. Wanafunzi sasa wameanza kutekeleza visomo hivyo vinavyohusiana na afya, hasa kukabiliana dhidi ya Ebola”, amesema mwalimu huyo.

Katika mji wa Niamey, mabango yamewekwa barabarani. Na kwenye mabango hayo kumekua kukiandikwa maeneo ya kuwasihi raia kutogusana hovyo kwa minajili ya kukabiliana na virusi vya Ebola: “Tuwe makini ! Sote pamoja, tuzuiye Ebola, usafi, tuoshe mikone, na somo hili liendelee”.

Kampeni hii ni moja ya mipango ya kitaifa ya kujilinda dhidi ya mambukizi ya magonjwa mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.