Ebola: WHO yapongeza jitihada zinazoendeshwa na nchi mbalimbali
Shirika la afya duniani, WHO limetoa takwimu mpya kuonesha idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola katika Mataifa ya Afrika Magharibi.
Imechapishwa:
WHO imesema idadi mpya ya watu waliopoteza maisha nchini Liberia , Guinea na Sireleon ni 4,818 wala sio 4,951 kama ilivyoripotiwa mwisho wa mwezi uliopita.
Shirika hilo limetoa pia takwimu mpya za maambukizi ambapo idadi imepungua kutoka watu 13,567 hadi 13,042.
Kati ya mataifa yaliyoathirika na Ebola, Liberia inaongoza kwa kuwa na watu wengi waliopoteza maisha ambao ni 2,697 huku 6,525 wakiwa wamelazwa wakiwa wamewekwa karantini, na inafuatwa na Sierra Leone, ambayo imepoteza watu 1,070.
WHO imesema sababu kubwa ya vifo kupungua ni jitihada zinazoendelea kuwahudumia wagonjwa wanaofika katika vituo vya afya kupata msaada.
Katika hatua nyingine, rais Barrack Obama amesema ataomba Bunge la Congress kupitisha mswada ili kuruhusu kutolewa kwa Dola bilioni 6 nukta 2 kusaidia kupambana na Ebola.