Pata taarifa kuu
MALI-Ebola-Afya

Ebola: hofu imetanda Mali

Hofu imetanda katika mji wa Kayes nchini Mali, ambapo msichana mdogo wa umri wa miaka miwili aliye fariki Ijumaa Oktoba 24 baada ya kuambukizwa virusi vya Ebola.

Hospitali ya mji wa Kayes, alikofariki mtoto wa umri wa miaka miwili aliye ambukizwa virusi vya Ebola.
Hospitali ya mji wa Kayes, alikofariki mtoto wa umri wa miaka miwili aliye ambukizwa virusi vya Ebola. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Ni mtu wa kwanza kubainika kuwa na virusi vya Ebola katika ardhi ya Mali tangu kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa huo katika baadhi ya mataifa ya Afrika ya Magharibi.

Viongozi wa Mali wameitaka tume ya matabibu iliyotumwa Kayes kubaki katika mji huo hadi pale itabainika kuwa hakuna dalili za ugonjwa huo katika eneo hilo.

“ Kwa kweli hofu imetanda katika mji wa Kayes. Mwanzoni inaeleweka, lakini hatuwezi kufumbia macho suala hili. Hofu imetanda sehemu zote. Hata rais wa Marekani Barack Obama anakerwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola. Raia wanapaswa kuhamasishwa na kuonyeshwa kua ugonjwa huo unashughulikiwa ”, amesema daktari Lamine Diarra, mshauri kwenye wizara ya afya.

Viongozi wa mji wa Kayes wamechukua hatua za kukabiliana na virusi vya Ebola. Raia wa mji huo hawasalimiani kwa kupeana mikono. Katika hoteli na majengo ya serikali hatua kali zimechukuliwa ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Ebola.

Raia 43 waliyomgusa mtoto huyo aliye fariki baada ya kuambukizwa virusi vya Ebola, wamewekwa karantini nje kidogo ya mji wa Kayes. Kwa mujibu wa daktari mmoja, miongoni mwa watu hao hakuna aliye ambukizwa virusi vya Ebola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.