Pata taarifa kuu

Pasaka: Katika ujumbe wake wa 'urbi et orbi', Papa Francis himiza amani

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ametoa ujumbe wake wa jadi "kwa jiji na kwa ulimwengu" siku ya Jumapili, Machi 31, akirejelea tena wito katika hali nyingi za migogoro na umaskini huko Gaza na Ukraine, lakini pia akielekeza macho yake kuelekea bara la Afrika.

"Tusiruhusu uhasama unaoendelea kuendelea kuathiri vibaya raia ambao sasa wamechoka, haswa watoto," Papa Francis amehimiza wakati wa baraka zake za "urbi et orbi" mnamo Machi 31, 2024.
"Tusiruhusu uhasama unaoendelea kuendelea kuathiri vibaya raia ambao sasa wamechoka, haswa watoto," Papa Francis amehimiza wakati wa baraka zake za "urbi et orbi" mnamo Machi 31, 2024. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Papa Francis amealika ulimwengu, Jumapili Machi 31, "kutokubali mantiki ya silaha" baada ya kulakiwa na umati wa waumini kwenye hafla ya sherehe za Pasaka huko Vatican, akiondoa wasiwasi wa saa za hivi karibuni juu ya kudhoofika kwa afya yake. "Tusiache uhasama unaoendelea uendelee kuathiri vibaya raia ambao sasa wamechoka, hasa watoto," amehimiza Papa mwenye umri wa miaka 87 wakati wa baraka zake za urbi et orbi ("kwa jiji na kwa ulimwengu").

Nchi nyingi zatajwa

Akitaja zaidi ya nchi kumi na mbili zilizo katika mtego wa vita wakati wa muhtasari mkubwa wa migogoro ya kimataifa, amebainisha kuwa mawazo yake yalikwenda "kwanza kabisa kwa waathiriwa wa migogoro mingi inayotokea ulimwenguni, kuanza na ile ya Israeli na Palestina, na ile ya Ukraine. Kristo afungue njia ya amani kwa wakazi waliofiwa wa maeneo haya. Wakati nikitoa wito wa kuheshimiwa kwa kanuni za sheria za kimataifa, natoa wito wa kubadilishana kwa jumla kwa wafungwa wote kati ya Urusi na Ukraine."

"Tusiruhusu upepo wa vita uvume Ulaya na eneo la Mediterania. Tusikubali mantiki ya matumizi ya silaha na kujihami tena na silaha," ameongeza. 

"Hata hivyo," Francis ameongeza, "natoa wito tena kwa upatikanaji wa misaada ya kibinadamu huko Gaza kuhakikishiwa, kwa mara nyingine tena kuhimiza kuachiliwa kwa haraka kwa mateka waliotekwa nyara Oktoba 7, pamoja na kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza. "

Katika Jumapili ya Pasaka, wakristo husherehekea ufufuo wa Yesu Kristo na hivyo ushindi wa uzima dhidi ya kifo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.