Mkutano wa baraza la mazingira unaendelea jijini Nairobi
Nairobi – Mawaziri wa mazingira na wadau mbambali kutoka zaidi ya nchi 180 wanakutana jijini Nairobi nchini Kenya, kwenye mkutano wa sita wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira UNEA, kujadili namna ya kuendelea kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Huku athari za mabadiliko ya hali ya hewa zikiendelea kuongezeka duniani, uchafuzi wa mazingira umeonekana kuwa sababu kuu ya vifo vya mapema duniani.
Watetezi wa mazingira sasa wanayataka mataifa kuzingatia zaidi sheria za mazingira ili kujikwamua kutoka kwa athari hizi. Leila Benali ni rais wa baraza la mazingira la Umoja wa Mataifa.
“Tuko katika wakati ambapo tunahitaji kurejesha imani miongoni mwa mataifa na imani katika ubinadamu na kile kilichosalia kwetu katika utu wa kuboresha mazingira.” alisema Leila Benali ni Rais wa baraza la mazingira la umoja wa mataifa.
Leila Benali ni Rais wa baraza la mazingira la umoja wa mataifa
Tayari malengo 19 yamependekezwa kwenye mkutano wa baraza la mazingira unaondelea jijini Nairobi,malengo hayo yakijumuisha uimarishaji wa kawi safi,kupunguza matumizi ya kemikali na kuangazia utaratibu wa kuchakata taka (Recycling.)
Inger Andersen ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la umoja wa mataifa kuhusu mazingira.
“Ni muhimu sana kwamba ulimwengu wote unajizatiti kuchukua hatua kuhusu mazingira, ili tuweze kukidhi malengo endelevu ambayo tuliahidi kila mmoja wetu mwaka 2015.”Inger Andersen ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la umoja wa mataifa kuhusu mazingira.
Inger Andersen ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la umoja wa mataifa kuhusu mazingira
Hata hivyo mashirika ya mazingira nayo yanaendelea kushinikiza wajumbe kupea teknolojia kipau mbele kuhepuka matumizi ya mafuta ya kisukuku ambayo yamechangua pakubwa uharibifu wa mazingira. Hawa ni baadhi ya watetezi wa mzingira.
Wanaharakati wa Mazingira nchini kenya
Zaidi ya wajumbe 7,000 wanaudhuria mkutano huo wa mazingira jijini Nairobi Kauli mbiu ikiwa hatua za kimataifa zenye ufanisi, na endelevu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Victor Moturi- RFI Kiswahili, Nairobi.