Pata taarifa kuu

UN yaonya juu viashiria vya mabadiliko ya hali ya hewa kuwa katika rangi nyekundu

Mwaka wa 2023 ndio mwaka wa joto zaidi kuwahi kurekodiwa na Shirika la Hali ya Hewa Ulimwenguni linaripoti kwamba rekodi za halijoto sio pekee ambazo zimevunjwa, "au hata kusambaratika". Chombo cha Umoja wa Mataifa kinachapisha ripoti yake ya kila mwaka "Hali ya tabianchi duniani" Jumanne hii, Machi 19, ambayo inatoa "maana mpya na ya kutisha kwa usemi "kuwa nje ya vigezo", licha ya mwanga wa matumaini.

Bango linaloonyesha halijoto ya nyuzi joto 118 Fahrenheit (nyuzi 47 Selsiasi) wakati wa wimbi la joto lililorekodiwa huko Phoenix, Arizona, Julai 18, 2023.
Bango linaloonyesha halijoto ya nyuzi joto 118 Fahrenheit (nyuzi 47 Selsiasi) wakati wa wimbi la joto lililorekodiwa huko Phoenix, Arizona, Julai 18, 2023. AFP - PATRICK T. FALLON
Matangazo ya kibiashara

Iwe kaboni dioksidi (CO2), methane (CH4) au oksidi ya nitrojeni (N2O), uzalishaji wa gesi chafuzi ulifikia viwango vya rekodi mnamo 2022, mwaka uliopita ambapo Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) lina data ya jumla. Data ya kwanza ya 2023 inaonyesha "ongezeko linaloendelea".

.
. © Studio graphique FMM

Gesi hizi za chafu hunasa joto katika angahewa na ndizo wahusika wakuu wa mabadiliko ya hali ya hewa. Hutokana na shughuli za binadamu, hasa mwako wa nishati ya mafuta, kilimo kikubwa au michakato ya viwanda, na hubakia hewani kwa miongo kadhaa (kwa mfano, miaka 100 kwa CO2). Kwa hivyo halijoto itaendelea kupanda kwa miaka mingi hata kama binadamu waliacha kutoa gesi hizi angani.

.
. © Studio graphique FMM

Mwaka jana, wastani wa joto duniani ulikaribia kikomo cha digrii +1.5 ikilinganishwa na miaka ya 1850-1900, hiyo ni kusema kabla ya mapinduzi ya viwanda na kuanza kwa uzalishaji mkubwa wa gesi chafu. Kikomo hiki kiliwekwa na mataifa duniani kote wakati wa mkutano wa tabia nchi, COP21, na Mkataba wa Paris mwaka 2015. Inaambatana kwa kizingiti zaidi ambacho njia zetu za maisha zinatishiwa. Kwa bahati nzuri, sio kwa kuzingatia rekodi za hali ya hewa kutoka kwa mwaka mmoja kwamba kizingiti hiki kinachukuliwa kuwa kilizidi lakini kwa kuchukua wastani kwa muda mrefu. "Wastani wa joto wa 2014-2023 wa miaka kumi ni digrii +1.2," inabainisha WMO. Mnamo mwaka 2023, "kuanzi mwezi Juni hadi Desemba imevunja rekodi zote za joto". Hii ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa lakini pia mfumo wa hali ya Hewa,  El Niño, tukio la asili na la mzunguko ambalo linaongeza zaidi halijoto duniani, ripoti inakumbusha.

.
. © Studio graphique FMM

Joto lililokusanyika katika bahari lilifikia kiwango chake cha juu zaidi katika miaka 65 ya uchunguzi mnamo mwaka 2023, kulingana na WMO. Mawimbi ya joto yaliyoenea yalipiga Atlantiki ya Kaskazini hasa, hasa mwishoni mwa mwaka, na joto linachukuliwa kuwa "kali " na wataalam, kutokana na joto kizidi 3 ° C juu ya wastani. Mawimi yalikuwa “makuwa na makali katika Mediterania kwa mwaka wa 12 mfululizo,” ripoti hiyo pia inabainisha. Kwa kuzingatia wingi mkubwa wa maji unaowakilisha bahari, kuyapa joto huchukua muda mrefu... lakini pia kuyapoza. Kwa hivyo, hata kama utoaji wa gesi chafuzi ukisimamishwa mara moja, ungechukua karne nyingi au hata milenia kwa kuyakupoza, inaonya WMO. Madhara yake ni kupanda kwa kina cha bahari pamoja na kuvurugika au kudhoofika kwa wanyama na mimea na athari kwa wakazi wanaoishi kwenye mwambao na uvuvi.

.
. © Studio graphique FMM

Mwaka jana, viwango vya bahari vilipanda kiasi hiki tangu rekodi za satelaiti zilipoanza mwaka 1993. Hata hivyo, "kuanzia mwezi Julai hadi Septemba 2023, dalili ya kuongezeka huku kwa El Niño inaonekana wazi". Ili kuelewa athari za mabadiliko ya tabinchi, kwa hiyo ni muhimu kuangalia mwenendo wa muda mrefu. Kwa hivyo, kiwango cha kupanda kwa kina cha bahari kiliongezeka kutoka 2.13 mm kwa mwaka mooha katika miaka ya 1990 hadi 4.77 mm katika miaka kumi iliyopita.

.
. © Studio graphique FMM

Ikiwa viwango vya bahari vinaongezeka, ni kwa sababu maji ya joto yanapanuliwa zaidi (yanachukua nafasi zaidi) kuliko maji baridi, lakini pia kwa sababu barafu za miti na milima zinayeyuka zaidi na zaidi, hali ambayo huongeza kiasi kikubwa cha maji katika bahari.

"Takwimu za awali zinaonyesha kwamba barafu duniani kote imepoteza kwa wastani sawa na mita 1.2 ya unene wa barafu mwaka 2023," kulingana na WMO. 

.
. © Studio graphique FMM

Data hizi zote za kisayansi hutafsiriwa kuwa matukio ya hali ya hewa kali mwaka wa 2023, ambayo WMO hufanya orodha ya kusikitisha. Katika Pembe ya Afrika, mafuriko baada ya ukame wa miaka mingi yamewakosesha makazi watu milioni 1.8. Nchini Libya, yaligharimu maisha ya karibu watu 10,000. Kimbunga Otis kilipiga mji wa mapumziko wa Mexico wa Acapulco, na kusababisha hasara ya kiuchumi inayokadiriwa kuwa karibu dola bilioni 15. Mawimbi ya joto kali yalipitia maeneo mengi ya dunia yenye mawimbi makubwa zaidi ya joto barani Ulaya na Afrika Kaskazini (50.4°C iliyorekodiwa huko Agadir nchini Morocco kwa mfano). Ukame pia unaongezeka, na kusababisha hasara ya mazao na ukosefu wa maji nchini Uhispania, Uruguay na Argentina. Msimu wa moto nchini Canada pia ulikuwa mbaya zaidi kuwahi kurekodiwa huku takriban hekta milioni 15 za msitu zikiteketea kwa moto.

.
. © Studio graphique FMM

"Majanga haya yanagharimu maisha ya binadamu, yanaharibu uchumi, yanahusishwa na majanga mengine kama vile migogoro ya ya ndani au vita, yanazidisha matatizo ya usalama wa chakula, kuhama kwa watu na athari kwa watu walio katika hatari," anabainisha Omar Badour, mkuu wa ufuatiliaji wa tabianchi duniani katika Shirika la Hali ya Hewa Ulimwenguni, WMO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.