Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa wazindua chombo cha kufuatilia uchimbaji wa mchanga baharini

Mchanga ni rasilimali inayotumika zaidi baada ya maji. Na kama maji, mustakabali wake unazua maswali. Je, mchanga unatishiwa na uchimbaji kupita kiasi? Hivi ndivyo Umoja wa Mataifa unabaini. Umoja wa Mataifa umezindua jukwaa kwa minajili ya kufanya vyema uchunguzi kuhusiana na uchimbaji mchanga baharini. Shughuli ambayo inatishia sio tu mfumo mzima wa ikolojia, lakini pia njia yetu ya maisha.

Uchimbaji na usafirishaji wa mchanga huko Allahabad, India, rasilimali inayotumika zaidi baada ya maji kwa shughuli mbalimbali za ujenzi, hapa mnamo ilikwa mwezi Oktoba 2007.
Uchimbaji na usafirishaji wa mchanga huko Allahabad, India, rasilimali inayotumika zaidi baada ya maji kwa shughuli mbalimbali za ujenzi, hapa mnamo ilikwa mwezi Oktoba 2007. AP - Rajesh Kumar Singh
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Geneva, Jérémie Lanche

Tani bilioni 50 za mchanga hutolewa kutoka kwa mazingira kila mwaka. Uchimbaji wa nyenzo hii umefikia idadi "kubwa". Lakini takwimu hii kubwa inalingana kabisa na mahali rasilimali hii imechukua maishani mwetu, anaeleza Pascal Peduzzi wa shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa: “Shule zenu, hospitali zenu, barabara zenu, mabwawa ya kuzalisha umeme kwa maji , mitambo ya upepo, paneli za jua, kioo. Kwa kweli, jamii yetu yote inategemea mchanga kama nyenzo ya ujenzi. »

Zaidi kidogo ya 10% ya mchanga unaochimbwa na binadamu hutoka baharini. China, Marekani, lakini pia Ubelgiji na Uholanzi ni miongoni mwa nchi zilizo na meli nyingi zaidi za uchimbaji, aina ya chombo kikubwa ambacho hukwangua chini ya bahari kutafuta mashapo. Pamoja na matokeo ambayo tunafikiria kwa mazingira. Na kwa ajili ya ulinzi wa rasilimali ambayo inaweza kuisha haraka sana: “Ubelgiji tayari imeona kwamba bado ina miaka 80 ya ujazo na uchimbaji wa mchanga kama ilivyo sasa. Tutaihitaji sana ili kulinda dhidi ya kupanda kwa viwango vya bahari. Kwa hiyo itakuwa nyenzo ya kuvutia sana kwa kukabiliana na mabadiliko yatabianchi. "

Kwa kukosekana kwa kanuni za kimataifa kuhusu biashara ya mchanga na uchimbajii, Umoja wa Mataifa umeunda jukwaa ambalo litawezesha kufuatilia meli za uchimbaji. Ili kuweza kutathmini vyema kiwango cha mchanga kinazopatikana. Na pia, kukemea vitendo vibaya kwa uchimbaji wa mchanga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.