Pata taarifa kuu

COP15: Makubaliano ya kihistoria kuhusu bayoanuwai yaidhinishwa Montreal

Baada ya mazungumzo ya saa nyingi, mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bioanuwai huko Montreal Jumatatu ulipitisha kanuni ya "mfumo wa kimataifa wa bioanuwai", ramani ya malengo 23 ya kujaribu kukomesha uharibifu wa asili ifikapo mwaka 2030.

Maafisa wa polisi wakipita kwenye kituo cha mikusanyiko kwenye kongamano la COP15 la Bayoanuwai Jumatano, Desemba 14, 2022 huko Montreal.
Maafisa wa polisi wakipita kwenye kituo cha mikusanyiko kwenye kongamano la COP15 la Bayoanuwai Jumatano, Desemba 14, 2022 huko Montreal. AP - Ryan Remiorz
Matangazo ya kibiashara

"Makubaliano yamepitishwa," amesema Huang Runqiu, rais wa China wa COP15, mjini Montreal usiku wa kuamkia Jumatatu.

Baada ya miaka minne ya mazungumzo magumu, siku kumi na usiku mmoja, zaidi ya mataifa 190 yamefikia makubaliano. "Mkataba huu wa amani na asili" unaoitwa "makubaliano ya Kunming-Montreal" unalenga kulinda ardhi, bahari na viumbe kutokana na uchafuzi wa mazingira, uharibifu na mgogoro wa Tabia nchi.

Nchi zimekubaliana juu ya ramani inayolenga kulinda asilimia 30 ya ardhi na bahari ifikapo mwaka 2030. Hili litafanyika “kupitia mitandao ya uwakilishi wa ikolojia, iliyounganishwa vyema na inayosimamiwa kwa usawa” na “huku ikihakikisha kwamba matumizi yoyote endelevu (. ..) yanaendana kikamilifu na malengo ya uhifadhi”. Lengo ni la kimataifa na si la kitaifa, ikimaanisha kwamba baadhi yao hufanya zaidi ya wengine, au kufanya zaidi juu ya nchi kavu kuliko baharini. Hizi 30% ni kiwango cha chini kwa wanasayansi na mashirika yasiyo ya kiserikali, ambao wanaamini kuwa 50% ingekuwa muhimu. Hadi sasa, 17% ya ardhi na 8% ya bahari zinalindwa.

Lengo la pili: kurejesha 30% ya mifumo ikolojia ya nchi kavu, bahari ya bara na mifumo ikolojia iliyoharibiwa ya pwani na baharini.

Mazungumzo hayo yameonyesha maelewano marefu kati ya Kaskazini na Kusini: matarajio zaidi ya kiikolojia badala ya ruzuku zaidi za kimataifa, na kinyume chake. Mwishowe, nakala hii inaidhinisha lengo la nchi tajiri kutoa "angalau dola bilioni 20 kwa mwaka ifikapo mwaka 2025, na angalau dola bilioni 30 kwa mwaka ifikapo mwaka 2030". Hiyo ni takriban maradufu na mara tatu ya msaada wa sasa wa kimataifa kwa bioanuwai.

  Lengo lingine ambalo halikupangwa au sio lazima kushinda mapema: kupunguzwa kwa viuatilifu. Makubaliano hayo yanalenga kupunguza "hatari za uchafuzi wa mazingira na athari mbaya za uchafuzi wa mazingira kutoka vyanzo vyote, kufikia mwaka 2030, hadi viwango ambavyo havina madhara kwa viumbe hai". Mapambano ya muda mrefu yamezikutanisha Umoja wa Ulaya dhidi ya nchi kama Brazil, India na Indonesia.

Lakini pia kuna udhaifu katika maandishi haya, anasisitiza mwandishi wetu maalum huko Montreal, Lucile Gimberg. Kama ukumbusho, karibu hakuna lengo lililowekwa katika makubaliano ya awali, mwaka 2010 huko Aichi, limepatikana mwishoni mwa 2020. Wakati huu, nchi zimepitisha utaratibu wa pamoja wa kupanga na ufuatiliaji, na viashiria sahihi. Utaratibu ambao bado utalazimika kujithibitisha. Maandishi yanasalia kuwa ya chini ya kisheria kuliko yale ya makubaliano ya Tabia nchi ya Paris.

Na kisha ni wazi kukatishwa tamaa kwa idadi fulani ya nchi za Kusini, hasa nchi za Afrika, juu ya ufadhili ambao unaongezeka, lakini ambao haukidhi matarajio yao.

Makubaliano ya 'kihistoria'.

Walakini, makubaliano haya yanaelezewa kama 'ya kihistoria' na Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen. 'Kihistoria' pia kwa Christophe Béchu, Waziri wa Mpito wa Ikolojia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.