Pata taarifa kuu

Shirika la maendeleo la Ufaransa AFD limefadhili sekta ya afya nchini Kenya

Nairobi – Nchini Kenya, Shirika la maendeleo la Ufaransa AFD linashirikiana  na Hospitali ya Agakhan  na ile ya Lumumba mjini Kisumu Magharibi mwa nchi hiyo kwa kufadhili ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi na watoto.

Madakatari katika hospitali ya Agahkan
Madakatari katika hospitali ya Agahkan © Florence Kiwuwa
Matangazo ya kibiashara

Kwenye hospitali ya Agakhan AFD imewekeza asilimia sabini katika ujenzi wa jengo jipya lililobeba vitengo tofauti tofauti kama vile vya upigaji picha wa mifupa ,wadi ya kinamama na hata vyumba spesheli vya wagonjwa waliopata ajali .

Vilevile shirika hilo limefadhili upanuzi wa hospitali ya Lumumba  na kununu vifaa vya matibabu ambavyo vimeruhusu kufunguliwa kwa kitengo cha upasuaji wa wanawake kipindi wanapojifungua.

Lengo kuu la  AFD ni kuimarisha afya ya wagonjwa  kwenye eneo hilo.

Loran Meme anahusika na sekta ya afya katika Shirika hilo.

"Hospitali hii ya kisumu itaweza kuhudumia hata hospitali  zingine na itaweza  pia kufikisha huduma za matibabu  kwa wanachi hata  wanaoishi mbali na Kisumu" .Alisema Loran Meme.

00:20

KENYA _Son Loran Meme : Agence française de dévelopment launches health programs in Western region

Rita Gashaghe , anayehusika na mauzo katika Hospitali ya Agakhan pia alieleza kuwa mradi huo umewasaidia kuongeza vitanda 46 zaidi na kufikisha vitanda 116 na amekuwa na kauli hii kufuatia msaada huo.

"Hapa Agakhan Kisumu tulikua na upanuzi wa jengo la matibabu na tumeongeza vitanda kutoka sabini sasa tumekua na vitanda 116 na pia tumeongeza huduma zaidi hata za waliopata ajali ".Alisema Rita Gashaghe.

00:29

KENYA _Son Rita Gashaghie : Agence française de dévelopment launches health programs in Western region

Wagonjwa katika hopsitali hizo mbili pia wameuzungumzia mradi huu na kusema kuwa wameupenda maana umewaisaidi pakubwa.Mengi zaidi tutakuletea kwenye Makala ya Siha Njema katika siku zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.