Pata taarifa kuu

Tabianchi: Vijana sita kutoka ureno wafungulia mashitaka nchi 32 mbele ya ECHR

Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu itachunguza siku ya Jumatano, Septemba 27, malalamiko ya vijana sita wa Ureno ambao wanashtaki nchi 32 kwa kutochukua hatua kuhusu tabia nchi, ikiwa ni mara ya kwanza jambo hilo kufanyika.

Moto wa majira ya joto ya mwaka 2017 nchini Ureno ulisababisha vifo vya watu 110.
Moto wa majira ya joto ya mwaka 2017 nchini Ureno ulisababisha vifo vya watu 110. REUTERS/Rafael Marchante
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa Claudia Duarte Agostinho, dada yake, kaka yake, jirani yake na marafiki wawili, wanasema siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu hatimaye imewadia. Miaka sita baada ya kuanza hatua zao za kisheria, malalamiko yao yanachunguzwa Jumanne hii na Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu. Wakiwa na umri wa miaka 11 hadi 24, walalamikaji walipata uzoefu wa karibu wa moto ambao uliteketeza makumi ya maelfu ya hekta na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 100 nchini mwao mnamo mwaka 2017. Maafa ambayo yaliwafanya kufahamu juu ya ongezeko la joto duniani, tabia nchi, na hamu kubwa ya kudai uwajibikaji.

"Serikali za Ulaya zinashindwa kutulinda," anasema André Oliveira, 15, mmoja wa watu sita waliowasilisha malalamiko yao. Yeye na wenzake wanashutumu mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya pamoja na Urusi, Uturuki, Uswisi, Norway na Uingereza kwa kutozuia vya kutosha utoaji wao wa gesi chafu, wakibaini kwamba hii inachochea ongezeko la joto duniani na kuathiri hali ya maisha na afya zao.

Kisheria, vijana sita wa Ureno wanadai ukiukaji wa "haki ya kuishi" na "haki ya kuheshimu maisha ya kibinafsi", iliyoainishwa katika Mkataba wa Ulaya wa Ulinzi wa Haki za Kibinadamu, hasa kuhusiana na ahadi za kimataifa zilizowekwa katika makubaliano ya Paris kuhusu tabia nchi mwaka wa 2015. Wakili wao, Gerry Liston, mwanachama wa Shirika lisilo la kiserikali la Uingereza Global Legal Action Network (Glan), anabaini kutoka kwa ECHR uamuzi "ambao utafanya kama mkataba wa lazima uliowekwa na Mahakama" kwa Mataifa na ataewahimiza "kuharakisha juhudi zao za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi". "Kwa mtazamo wa kisheria, itakuwa ni kutakuwa mabadiliko makubwa," amesema, wakati huko Ulaya kama mahali pengine mahakama zinazidi kuombwa dhidi ya kushindwa kwa serikali kuhusu tabia nchi au sera za uchafuzi za makampuni .

Huko Strasbourg, ambako ECHR ina makao yake, kesi hiyo inachukuliwa kwa uzito: ikiainishwa kama “kipaumbele”, itajadiliwa pia mbele ya muundo mzito zaidi wa Mahakama, Baraza Kuu, linalojumuisha majaji 17. Kwa sababu ikiwa ECHR imetoa, katika miongo mitatu iliyopita, maamuzi mengi kuhusiana na mazingira, hii ni mara ya kwanza kwa kukazia hasa ongezeko la joto duniani.

Lakini kabla ya kutoa uamuzi kuhusu uhalali huo, Mahakama itachunguza kwanza kukubaliwa kwa ombi hilo, jambo ambalo linaashiria uzingatiaji wa vigezo vikali ambavyo kesi nyingi zilisambaratika huko nyuma, ikiwamo katika masuala ya mazingira. Na katika mashauri yaliyoletwa na Wareno sita, swali hilo linapaswa kujadiliwa vikali. Kwa kawaida ECHR huhitaji kwamba walalamikaji wawe wamewasilisha malalamiko yao mbele ya mahakama za kitaifa kabla ya kuiomba iingilie kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.