Pata taarifa kuu

Mkutano wa Kilele kuhusu tabianchi Afrika, mkutano wa kwanza muhimu kwa kuzingatia COP28

Pamoja na "Mkutano wa kwanza wa tabianchi Afrika", Nairobi Jumatatu inaanza miezi minne yenye shughuli nyingi zaidi kwa mwaka kwa mazungumzo ya kimataifa kuhusu hali ya hewa, na utahitimishwa na vita vya kumaliza nishati chafu kwenye mkutano wa COP28 huko Dubai mnamo mwezi Desemba.

Moja ya maeneo barani Afrika yaliyoathirika na ukame kutokana na mabadiliko ya tabia nchi
Moja ya maeneo barani Afrika yaliyoathirika na ukame kutokana na mabadiliko ya tabia nchi Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa muda wa siku tatu, baadhi ya viongozi ishirini na maafisa kutoka Afrika na kwingineko, akiwemo mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, watakaribishwa katika mji mkuu wa Kenya na Rais William Ruto, ambaye anatumai kuwa mkutano huu utaliruhusu bara hilo kupata lugha moja juu ya maendeleo na tabianchi ili "kupendekeza masuluhisho ya Afrika" katika mkutano ujao wa Umoja wa Mataifa wa tabianchi.

Katika dunia ambayo iko nyuma sana katika malengo yake ya kupunguza utoaji wa hewa chafu unaosababisha ongezeko kubwa la joto duniani kwa raia, mazungumzo kabla ya mkutano wa COP28, yaliyoongozwa mwaka huu na shirika la nishati ya mafuta na gesi ya Umoja wa Falme za Kiarabu, yanaonyeshwa na upinzani mkali dhidi ya nishati ya baadaye ya binadamu.

Kando na viongozi wengine wa Afrika, Ruto amejaribu kuangazia uwezo wa Afrika kama nguvu ya kijani kibichi kiviwanda na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufungua fedha kwa ajili ya bara hilo.

"Walionyesha wazi kuwa Afrika haikuwa mwathirika, lakini mhusika muhimu katika kutatua mgogoro wa tabianchi duniani kupitia ukuaji wa kijani," Mavis Owusu-Gyamfi, naibu kiongozi wa Kituo cha Mabadiliko ya Kiuchumi barani Afrika (ACET) ameliambia shirika la habari la AFP.

Mafanikio mjini Nairobi yangeongeza kasi kwa mikutano kadhaa muhimu ya kimataifa kabla ya COP28, kuanzia na mkutano wa kilele wa G20 nchini India na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba, na kisha mkutano wa kila mwaka wa Benki ya Dunia na shirika Fedha la Kimataifa (IMF) mwezi Oktoba huko Marrakech.

Ili kupunguza ongezeko la joto duniani hadi +1.5°C ikilinganishwa na enzi ya kabla ya viwanda vilivyotolewa na mkataba wa Paris, uwekezaji lazima ufikie dola bilioni 2,000 kwa mwaka katika nchi hizi ndani ya muongo mmoja, ilikokotoa IMF. Rasimu ya "Tamko la Nairobi" iliyoshauriwa na AFP, lakini bado uko chini ya mazungumzo, inaangazia "uwezo wa kipekee wa Afrika kuwa sehemu muhimu ya suluhisho".

Hati hiyo inataja uwezo mkubwa wa nishati mbadala wa eneo hilo, nguvu kazi yake changa na mali yake ya asili, ikijumuisha 40% ya akiba ya ulimwengu ya cobalt, manganese na platinamu, muhimu kwa betri na haidrojeni. Pia inajumuisha ahadi ya kuongeza mara tatu uwezo wa nishati mbadala katika bara, kutoka 20% ya umeme mwaka 2019 hadi 60% ifikapo 2030.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.