Pata taarifa kuu

Tabianchi: 'Mwaka 2024 utakuwa mwaka wa joto zaidi katika historia' (UN)

Kuna "uwezekano mkubwa" kwamba 2024 utakuwa mwaka wa joto zaidi katika rekodi, Umoja wa Mataifa umesema siku ya Jumanne. "Hatuwezi kusema kwa uhakika," lakini "ningesema kuna uwezekano mkubwa kwamba mwaka 2024 utavunja tena rekodi ya mwaka 2023," Omar Baddour wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO)amesema wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya kila mwaka ya hali ya hewa. 

[Picha ya kielelezo] Mwaka wa 2023 ndio wenye joto zaidi kuwahi kurekodiwa kufikia sasa. Hapa, mfanyakazi wa kujitolea wa WYD anatumia feni kupata hewa nzuri baada ya kupigwa na joto kali kabla ya kuwasili kwa Papa huko Lisbon, Agosti 6, 2023.
[Picha ya kielelezo] Mwaka wa 2023 ndio wenye joto zaidi kuwahi kurekodiwa kufikia sasa. Hapa, mfanyakazi wa kujitolea wa WYD anatumia feni kupata hewa nzuri baada ya kupigwa na joto kali kabla ya kuwasili kwa Papa huko Lisbon, Agosti 6, 2023. AP - Armando Franca
Matangazo ya kibiashara

Mwaka jana, wastani wa joto duniani ulikaribia kikomo cha digrii +1.5 ikilinganishwa na miaka ya 1850-1900, hiyo ni kusema kabla ya mapinduzi ya viwanda na kuanza kwa uzalishaji mkubwa wa gesi chafu. Kikomo hiki kiliwekwa na mataifa duniani kote wakati wa mkutano wa tabia nchi, COP21, na Mkataba wa Paris mwaka 2015. Inaambatana kwa kizingiti zaidi ambacho njia zetu za maisha zinatishiwa. Kwa bahati nzuri, sio kwa kuzingatia rekodi za hali ya hewa kutoka kwa mwaka mmoja kwamba kizingiti hiki kinachukuliwa kuwa kilizidi lakini kwa kuchukua wastani kwa muda mrefu. "Wastani wa joto wa 2014-2023 wa miaka kumi ni digrii +1.2," inabainisha WMO. Mnamo mwaka 2023, "kuanzi mwezi Juni hadi Desemba imevunja rekodi zote za joto". Hii ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa lakini pia mfumo wa hali ya Hewa,  El Niño, tukio la asili na la mzunguko ambalo linaongeza zaidi halijoto duniani, ripoti inakumbusha.

Iwe kaboni dioksidi (CO2), methane (CH4) au oksidi ya nitrojeni (N2O), uzalishaji wa gesi chafuzi ulifikia viwango vya rekodi mnamo 2022, mwaka uliopita ambapo Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) lina data ya jumla. Data ya kwanza ya 2023 inaonyesha "ongezeko linaloendelea".

Ikiwa viwango vya bahari vinaongezeka, ni kwa sababu maji ya joto yanapanuliwa zaidi (yanachukua nafasi zaidi) kuliko maji baridi, lakini pia kwa sababu barafu za miti na milima zinayeyuka zaidi na zaidi, hali ambayo huongeza kiasi kikubwa cha maji katika bahari.

"Takwimu za awali zinaonyesha kwamba barafu duniani kote imepoteza kwa wastani sawa na mita 1.2 ya unene wa barafu mwaka 2023," kulingana na WMO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.