Pata taarifa kuu

Marufuku ya matumizi ya plastiki kwa mara moja nchini Somalia

Somalia itapiga marufuku matumizi, uagizaji na utengenezaji wa plastiki ya matumizi kwa mara moja kuanzia Juni 30, Wizara ya Tabianchi imetangaza siku ya Alhamisi, ikitaja "athari zake mbaya" kwa mazingira.

Wakati chupa za plastiki zikiokotwa kwenye nyavu za wavuvi.
Wakati chupa za plastiki zikiokotwa kwenye nyavu za wavuvi. © Pixabay_CC0_MatthewGollop
Matangazo ya kibiashara

 

Wizara imetangaza "kusitishwa kabisa kwa uagizaji, usafirishaji, uzalishaji, biashara na matumizi ya mifuko ya plastiki ya matumizi mara moja kuanzia Juni 30, 2024", huku ikihimiza "makampuni na wafanyabiashara kutafuta ubunifu unaochukua nafasi ya plastiki na kulinda mazingira.

Mamlaka huko Mogadishu imechukua uamuzi huu "baada ya kuona athari mbaya za mifuko ya plastiki" katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika, mojawapo ya nchi zisizoendelea zaidi duniani. Katika bara la Afrika, zaidi ya nchi thelathini zinapiga marufuku au kupunguza uzalishaji, uingizaji au usambazaji wa kibiashara wa plastiki ya matumizi ya mara moja, kulingana na Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UNEP).

Mfano wa Rwanda, ambapo mifuko ya plastiki imepigwa marufuku kwa zaidi ya muongo mmoja, inachukuliwa kuwa mojawapo ya mafanikio makubwa zaidi. Uzalishaji wa kila mwaka wa mifuko ya plastiki duniani umeongezeka zaidi ya mara mbili katika miaka ishirini na kufikia tani milioni 460. Inaweza kuongezeka mara tatu ifikapo 2060 ikiwa hakuna kitakachofanyika. Hata hivyo, ni 9% tu ya plastiki ambayo inarejelewa.

Plastiki pia ina jukumu katika ongezeko la joto duniani: iliwakilisha 3.4% ya uzalishaji wa hewa duniani mwaka 2019, takwimu ambayo inaweza zaidi ya mara mbili ifikapo 2060, kulingana na OECD. Plastiki, kutoka kwa kemikali za petroli, iko kila mahali: taka ya ukubwa wote tayari inapatikana chini ya bahari na juu ya milima. Microplastics imegunduliwa katika damu au maziwa ya mama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.