Pata taarifa kuu
DRC-Jamhuri ya Afrika ya KAti-BEMBA-Sheria

ICC: Bemba akabiliwa na mashtaka

Kesi ya makamu wa zamani wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jean-Pierre Bemba, imefikia tamati kwenye Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.

Upande wa mashtaka kwenye kesi ya Jean-Pierre Bemba ukisikilizwa kwenye Mahakama ya ICC. Jumatano Novemba 12 mwaka 2014.
Upande wa mashtaka kwenye kesi ya Jean-Pierre Bemba ukisikilizwa kwenye Mahakama ya ICC. Jumatano Novemba 12 mwaka 2014. AFP PHOTO / POOL / BART MAAT
Matangazo ya kibiashara

Jean-Pierre Bemba anatuhumiwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Kesi yake ilianza kusikilizwa tangu mwaka wa 2010. Alikamatwa mwaka 2008, na mashtaka dhidi yake yaliwasilishwa kwenye Mahakama ya ICC mwaka 2009.

Jumatanu Novemba 12 majaji wa ICC wamesikiliza upande wa mashtaka.

Hoja za upande wa mashtaka zilianza kusikilizwa kwenye saa 4 saa za kimataifa, ambapo upande wa mashtaka umesikilizwa kwa muda wa saa moja na nusu. Hata hivo kabla ya hoja hizo majaji walianza kikao hicho cha leo kwa kueleza ratiba ya siku hizi mbili za kutamatika kwa kesi, mbele ya makamu wa zamani wa rais wa Congo Jean-Pierre Bemba.

Upande wa mashtaka umerejelea uhalifu uliyotekelezwa na wapiganaji wa kundi la waasi la MLC dhidi ya raia wa kawaida wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

“ Tuko mbele yenu ili kuwaomba mtuhumiwa atambuliwe kama muhusika wa mateso waliyoyapata raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati”, amesema mwakilishi wa Ofisi ya mwendesha mashtaka, Jean-Jacques Badibanga.

Upande wa mashtaka umesema wapiganaji wa MLC walio kuwa wakiongozwa na Jean-Pierre Bemba walisikika wakizungumza lugha ya Lingala ambayo inazungumzwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, walitambuliwa pia kwa sare zao walio kuwa wakivaa. Inasadikiwa kuwa wapiganaji hao wa Jean-Pierre Bemba walitekeleza uhalifu huo katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, na katika miji mingine kaskazini mwa nchi kama Bossangoa na Bozum.

Kesi hiyo imehudhuriwa kama kawaida na wafuasi wa chama cha Jean-Pierre Bemba cha MLC, huku wakiituhumu timu ya Mwendesha mashtaka kuwa inadanganya. Kwa mujibu wa wafuasi hao ni vigumu upande wa mashtaka kujua hali hali iliyo kua ikijiri katika uwanja wa mapigano, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Siku ya mwisho ya kutamatika kesi hiyo ni Alhamisi novemba 13.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.