Pata taarifa kuu
KENYA-UGAIDI-USALAMA

Shambulio jipya latokea Mandera

Siku kumi baada ya shambulio lililoendeshwa dhidi ya basi moja, shambulio jipya limetokea katika eneo la Mandera kaskazini mwa Kenya kwenye mpaka na Somalia. Watu 36  wameuawa katika shambulio hilo, Shirika la msalaba mwekundu limethibitisha.

Wapiganaji wa kundi la Al Shabab wakati wa mafunzo ya kijeshi.
Wapiganaji wa kundi la Al Shabab wakati wa mafunzo ya kijeshi. AFP/TOPSHOTS/STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limetokea usiku wa Jumatatu Desemba 1 kuamkia Jumanne Desemba 2 katika eneo la Karomey kwenye umbali wa kilomita zaidi ya kumi na tano na Mandera. Shambulio hilo limetokea karibu na eneo la Arabyia ambapo abiria 28 waliokua ndani basi waliuawa siku kumi ziliyopita.

Shambulio la sasa limeendeshwa na watu waliojifananisha na wachimba migodi katika migodi ya makampuni ya ujenzi. Watu hao walikua wakilala katika hema zao kwenye eneo ambapo hakuna umeme.

Kawaida watu wanaoendesha shughuli hiyo ya kuchimba migodi ni kutoka jamii ya Kikuyu, Kamba,Luo au Luhya, na wengi wao ni kutoka jamii ya Wakristo. Ushahidi mpya unaonesha kuwa washambuliaji hao wamekua wanajua eneo hilo kama limekua likitumiwa na wafanyakazi wanaochimba mawe kutoka jamii hizo.

Taarifa kutoka Ikulu ya Kenya imesema kuwa manusura wacahche wamezungumzia kuwa wamewaona magaidi ishirini miongoni mwa watu waliowashambulia.

Inaonekana kwamba, kama ilivyo kuwa katika mashambulizi ya awali, huenda washambuliaji waliwatenganisha Waislam na Wakristo. Wengi wa waliouawa walipigwa risasi kichwani. Kwa mujibu wa kiongozi wa Shirika la msalaba mwekundu, Abbas koromeo, ambaye ametembelea eneo la tukio, miili ya watu waliouawa imehifadhiwa katika kambi ya jeshi ya Mandera ili iweze kusafirishwa kwa ndege.

Mauaji haya yanatokea wakati hivi karibuni, serikali ya Kenya imekua ikikosolewa kushindwa kukabiliana na tishio la kigaidi. Kwa muda wa miezi kadhaa, wito umekua ukitolea wa kutaka Waziri wa mambo ya ndani na mkuu wa polisi wajiuzulu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.