Pata taarifa kuu
KENYA-SOMALIA-AL SHEBAB-MAUAJI-SHAMBULIO-USALAMA

Kenya: jeshi ladai kuwaua wapiganaji 100 wa Al Shabab

Serikali ya Kenya imethibitisha kuwa wanajeshi wake wamefanikiwa kuwaua wapiganaji 100 wa kundi la kigaidi la Al-Shabab, katika operesheni mbili tofauti zilizofwatia mauaji ya watu 28 Jumamosi Novemba 22.

Kikosi cha wanajeshi wa Kenya katika operesheni ya kutokomesha kundi la Al Shabab mjini Nairobi.
Kikosi cha wanajeshi wa Kenya katika operesheni ya kutokomesha kundi la Al Shabab mjini Nairobi. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Abiria 28 waliuawa mapema Jumamosi Novemba 22 asubuhi katika shambulio lililotokea nchini Kenya karibu na mpaka wa Somalia. Abiria hao waliyokuwa ndani ya basi walishambuliwa na wanamgambo wa Al shabab kutoka Somalia, ambao walikiri kutekeleza shambulio hilo.

Wanamgambo hao waliwakata vichwa abiria ambao hawakua “waislam”.

Shambulio hilo lilitokea saa 11 na dakika 45 asubuhi, wakati basi hilo likitokea Mandera, mji ambao unapatikana kati ya Kenya, Somalia na Ethiopia, katika eneo la Arabia.

Inasadikiwa kuwa basi lililazimika kusimama, kwani lilikua likilengwa kwa risasi na kusababisha watu wengi waliokua ndani ya basi hilo kujeruhiwa. Wauaji hao waliwatenganisha abiria Waislam na wasio Waislam, na baadae kuanza kushambulia abiria wasio Waislam, ambao wengi wao walikua walimu wakirudi makwao kusheherekea sikukuu ya Krismasi, wafanyakazi wa sekta ya afya, watumishi wa umma. Jumla ya abiria 28 wakiwemo wanawake 9, kwa mujibu wa mkuu wa polisi ya Kenya, David Kimaiyo, wameuawa.

Jumamosi mchana, shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya lilithibitisha idadi hiyo. Timu za

Utaratibu uliyotumiwa kwa kuwaua abiria hao ni sawa na ule uliyotumiwa Mpeketoni katika eneo la Lamu mwezi Juni na Julai ambapo washambuliaji waliwataka watu kutamka nguzo ya kwanza ya uislam "Shahada". Lakini wakati huo, wanaume ndio waliolengwa, wanawake hawakulengwa.

Kundi la Al Shabab lilikiri kutekeleza shambulio hilo, likibaini kwamba operesheni hiyio ni ulipizaji kisase dhidi ya opereshi ya polisi iliyoendeshwa hivi karibuni katika mji wa Bandari ya Mombasa, operesheni ambayo ililenga Misikiti kadhaa iliyochukuliwa kama inafunza imani kali za kidini. Wakati huo mamia ya waislam walikamatwa katika operesheni hiyo ya polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.