Pata taarifa kuu

Burkina Faso: TV5 Monde pamoja na vyombo vingine sita vya habari vyafungiwa matangazo

Baraza la Juu la Mawasiliano nchini Burkina Faso (CSC) linaendelea kuviwekea vikwazo vyombo vya habari ambavyo vilitaja ripoti ya Human Rights Watch ambayo inalishutumu jeshi kwa kuua zaidi ya raia 220 katika vijiji viwili mwezi wa Februari mwaka huu. 

Nembo ya sehemu ya habari ya kituo cha TV5 Monde.
Nembo ya sehemu ya habari ya kituo cha TV5 Monde. TV5 Monde
Matangazo ya kibiashara

CSC imeamua kusimamisha matangazo ya kituo cha televisheni ya TV5 Monde kwa wiki mbili, na kuzuia ufikiaji wa tovuti yake na vile vile tovuti za vyombo vingine sita vya habari: magazeti ya Ufaransa "Ouest France" na "Le Monde", Gazeti la kila siku la Uingereza "The Guardian" , idhaa ya Ujerumani Deutsche Welle, shirika la habari la Senegal la APAnews na wshirika la habari la EcoFin lenye makao yake nchini Cameroon na Uswisi.

Vyombo hivi vya habari vinashutumiwa kwa kuchapisha "taarifa za kijasusi na zenye mwelekeo" dhidi ya jeshi. Mwishoni mwa juma lililopita, BBC na Sauti ya Amerika zilifungiwa matangazo. 

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, CSC "inaalika vyombo vyote vya habari kuacha kusambaza" maudhui haya, chini ya adhabu ya vikwazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.