Pata taarifa kuu

Ukraine: Kamanda mkuu wa majeshi akiri kuzorota kwa hali katika uwanja wa vita

Urusi inaendelea na mashambulizi yake mashariki mwa Ukraine, na haswa katika eeo la Pokrovsk katika mkoa wa Donetsk, ambapo Kamanda Mkuu Oleksandr Syrsky anatambua kuwa kuna askari wa Ukrane wanaotoroka jeshi wakiwa vitani.

Kamanda mkuu wa majeshi ya Ukraine, Oleksandr Syrsky (kushoto) pamoja na mkuu wa idara ya ujasusi wa Ukraine Kirilo Budanov, Februari 9, 2024 huko Kyiv.
Kamanda mkuu wa majeshi ya Ukraine, Oleksandr Syrsky (kushoto) pamoja na mkuu wa idara ya ujasusi wa Ukraine Kirilo Budanov, Februari 9, 2024 huko Kyiv. AP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Kyiv, Emmanuelle Chaze

"Hali imezidi kuwa mbaya katika uwaja wa vita" haya ni maneno yaliyoshirikiwa kwenye mitandao yake ya kijamii na kamanda mkuu wa majeshi ya Ukraine Oleksandr Syrksy. Anazungumzia maendeleo ya kimkakati ya wanajeshi wa Urusi kwenye vijiji vitatu vya eneo la Pokrovsk katika mkoa wa Donetsk, ambapo hadi brigedi nne za Urusi ziliripotiwa kutumwa kujaribu kulishinda jeshi la Ukraine.

Syrsky anakubali kurudi nyuma kwa wanajeshi wake kutoka kwa baadhi ya maeneo lakini anazungumza juu ya hali ya nguvu katika siku za hivi karibuni ambayo imeona mafanikio kadhaa ya busara kwa Urusi, lakini katika maeneo mengine, bado kulingana na yeye, ngome za wanajesi wa Ukraine zimeboreshwa. Licha ya majaribio ya Urusi, jeshi la Ukraine bado linashikilia daraja huko Krinky, kwenye ukingo unaokaliwa wa Dnipro, karibu na Kherson.

Kabla ya msaada wa Marekani kuwasili nchini Ukraine, Taasisi yenye makao yake mjini Washington ya Utafiti wa Vita inakadiria kuwa vikosi vya Urusi vitapata mafanikio ya kimbinu katika wiki zijazo, bila ya kulisambaratisha jeshi la Ukraine.

Kwa upande wake, mkuu wa idara ya ujasusi wa Ukraine Kyrylo Budanov anaonya kuhusu wiki ngumu na mashambulizi mapya ya Urusi ambayo yanaweza kuikumba Ukraine mwanzoni mwa majira ya joto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.