Pata taarifa kuu

Mali: Mahakama ya Katiba inadai uwajibikaji kwa mishahara ya wajumbe wa CNT

Nchini Mali, fidia na marupurupu yaliyopokelewa na wanachama wa Baraza la Kitaifa la Mpito (CNT) yamezua utata mkubwa tangu mwanzoni mwa wikendi hii. Katika uamuzi wa Aprili 18 lakini uliwekwa wazi siku ya Alhamisi hii, Aprili 25, Mahakama ya Katiba inahitaji ufafanuzi kuhusu sheria mpya ambayo inadhibiti mishahara ya washauri wa taasisi hii.

Rais wa Baraza la Kitaifa la Mpito la Mali, Malick Diaw (katikati), akiwa na wajumbe wa CNT mjini Bamako mnamo Februari 2022.
Rais wa Baraza la Kitaifa la Mpito la Mali, Malick Diaw (katikati), akiwa na wajumbe wa CNT mjini Bamako mnamo Februari 2022. AFP - FLORENT VERGNES
Matangazo ya kibiashara

"Kutawala ni kutumikia umma, rudisheni pesa." Kwenye mitandao ya kijamii, sauti nyingi zinakosoa manufaa yanayotolewa kwa wanachama wa Baraza la Kitaifa la Mpito (CNT). CNT, chombo cha kutunga sheria cha mpito, kimechukua nafasi ya Bunge la Kitaifa nchini Mali kwa karibu miaka minne, lakini wajumbe wake hawajachaguliwa, kwa sababu wanachaguliwa na kuteuliwa kwa amri na mamlaka ya kijeshi.

Miongoni mwa sauti zilizotolewa ni ile ya kundi kubwa zaidi la vyama vya siasa vya Mali. Kundi hili - katika taarifa kwa vyombo vya habari - linasema limekerwa kwa marupurupu makubwa na fidia, inayopakana na uchafu, inayotolewa kwa nji isiyo halali.

Baada ya kupitishwa kwa kura miezi mitano iliyopita, Novemba 16, 2023, wakati wa kikao cha faragha, sheria hii hutoa gharama za uwakilishi, kodi za nyumba, posho za madereva, posho za matumizi ya kimsingi, na hata mgao wa mafuta kwa wanachama wote wa CNT.

Mambo yanayochukuliwa kuwa ya kawaida, lakini katika muktadha wa sasa ambapo wananchi wa Mali wanaombwa kuwa wastahimilivu katika kukabiliana na kukatika kwa umeme, gharama kubwa ya maisha na ukosefu wa usalama, hii inaonekana na wengi kama dhuluma. Washauri kadhaa wa CNT wanaelezea lawama hizi kama "mashambulizi ya kisiasa".

Faranga za CFA milioni kumi na tatu

Wakihojiwa na RFI, mmoja wao anakumbusha kwamba malipo haya yanatoka kwa bajeti ya taasisi, zaidi ya faranga za CFA milioni kumi na tatu kulingana na sheria ya fedha ya mwaka 2023, na kwamba hakuna ongezeko au fidia mpya iliyotolewa kwao. Kulingana na yeye, hatua hiyo inaruhusu, kinyume chake, uwazi zaidi katika usimamizi wa fedha za umma kwa vile inahalalisha utaratibu ambao umekuwepo kwa miaka mingi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.