Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA-MANDELA-KUMBUKUMBU-SIASA

Mandela, mwaka mmoja akiitoka dunia

Ni mwaka mmoja sasa tangu aitoke dunia rais wa zamani wa Afrika Kusini hayati Nelson Mandela Madiba, ambaye alifariki Desemba 5 mwaka 2013, akiwa na umri wa miaka 95. Maadhimisho ya kumbukumbu yatafanyika Ijumaa Desemba 5 nchini kote.

Sherehe ya kumbukumbu ya kifo cha Nelson Mandela Madiba baada ya mwaka mmoja shuja huyo wa taifa kuitoka dunia Desemba 5 mwaka 2014, Pretoria, Afrika Kusini.
Sherehe ya kumbukumbu ya kifo cha Nelson Mandela Madiba baada ya mwaka mmoja shuja huyo wa taifa kuitoka dunia Desemba 5 mwaka 2014, Pretoria, Afrika Kusini. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Afrika kusini , raia bado wana kumbukumbu ya tarehe 5 Desemba siku ya Alhamisi, ambapo rais Jacob Zuma alizungumza moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa. Ilikuwa saa 5 usiku saa za Afrika Kusini wakati ambapo alitangaza kifo cha Nelson Mandela Madiba.

Saa chache baadae mamia kwa maelfu ya raia walikusanyika mbele ya makaazi ya Madiba katika kata ya Houghten, eneo lenye mandhari nzuri mjini Johannesburg, huku wengine wakikusanyika katika makaazi yake alikoanza kuishi, mjini Soweto, eneo kulikoanzishwa harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Kadri muda ulivyokua ukisonga mbele ndivyo watu walivyokua wakitoa salaam za rambirambi na wengine kuweka shada za maua katika makaazi yake. Maelfu ya raia walikuja kutoa heshima zao za mwisho, wakiwemo marais na viongozi mbalimbali wa serikali.

Afrika Kusini inaadhimisha kumbukumbu ya kifo cha shujaa wa taifa Nelson Mandela Madiba, mwaka mmoja baadaye. Raia wa Afrika Kusini wametakiwa kupiga kengele na ala mbalimbali za muziki kwa muda wa dakika sita na sekunde saba. Dakika sita na sekunde saba zinaashiria miaka 67 ya harakati na mapambano ya kisiasa dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.