Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-GBAGBO-NGESSAN-FPI-UCHAGUZI-SIASA

Chama cha FPI chakabiliwa na malumbani

Nchini Côte d’Ivoire, mvutano umeendelea kujitokeza katika chama cha FPI cha Laurent Gbagbo, baada ya vyombo vya sheria vya nchini Côte d’Ivoire kuchukua uamzi wa kuahirisha mkutano uliyokua ulipangwa kufanyika Alhamisi Desemba 11 mwaka 2014. 

Laurent Gbagbo, mwenyekiti wa zamanai na mwasisi wa chama cha FPI (kushoto) na Pascal Affi N'Guessan, mwenyekiti wa FPI anaye maliza muda wake (kulia).
Laurent Gbagbo, mwenyekiti wa zamanai na mwasisi wa chama cha FPI (kushoto) na Pascal Affi N'Guessan, mwenyekiti wa FPI anaye maliza muda wake (kulia). Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ilichukua uamzi huo kwa ombi la kiongozi wa chama hicho Pascal Affi N’Guessan.

Kwa sasa mvutano umeendeleea kujitokeza na huenda machafuko ya katokea kati ya wafuasi wa kiongozi wa chama, Affi N'Guessan na rais wa zamani wa Côte d’Ivoire, Laurent Gbagbo. Pande hizo mbili zimejielekeza mahakamani leo Jumatatu Desemba 15 asubuhi ili kujua iwapo mkutano huo utafanyika hivi karibuni au la.

Leo Jumatatu Desemba 15, Pascal Affi N'Guessan, kiongozi wa chama na Agnes Monnet, msemaji wake wamewekwa kando na Sébastien Dano Djédjé. Kwa utaratibu huu wa dharura, Djédjé ambaye anahusika na maandalizi ya mkutano atajaribu kubatilisha kuahirishwa kwa mkutano huo.

Akihojiwa na RFI, Djédjé amesema hatokubali chama cha FPI kisambaratishwe.
"Congress yetu iliahirishwa kwa muda usiojulikana bila hata sisi kupewa taarifa. Kama hatuwajibiki, uamzi huu wa kukataza kufanyka kwa mkutano unaweza ukadumu kwa miaka kadhaa. Maslahi ya chama yatakua yametupwa kapuni", amesema Djédjé.

Hata hivyo Pascal Affi N’Guessan anataka mwanga utolewe kuhusu kugombea kwa Laurent Gbagbo kwenye uongozi wa chama cha FPI. Kwa sasa suala hilo lijko mikononi mwa Mahakama na litajadiliwa Alhamisi Desemba 18 mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.