Pata taarifa kuu
TUNISIA-Uchaguzi-Siasa

Beji Caïd Essebsi achaguliwa kuwa rais wa Tunisia

Tangu mapema Jumatatu Desemba 22 mchana Tunisia imempata rais npya. Beji Caïd Essebsi, kiongozi wa hcama cha Nidaa Tounes amemshinda mshindani wake, Moncef Marzouki.

Beji Caid Essebsi amechaguliwa kuwa rais wa Tunisia, Desemba 22, 2014, licha ya wale wanao mtuhumu kuwa na uhusiano na utawala wa Ben Ali.
Beji Caid Essebsi amechaguliwa kuwa rais wa Tunisia, Desemba 22, 2014, licha ya wale wanao mtuhumu kuwa na uhusiano na utawala wa Ben Ali. REUTERS/Zoubeir Souissi
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na matokeo rasmi, Waziri mkuu wa zamani BCE, amepata asilimi 55.68 za kura dhidi ya asilimia 44.32 za kura alizopata rais anaye maliza muda wake, Moncef Marzouki.

Beji Caïd Essebsi, anakua rais wa kwanza kuchaguliwa nchini Tunisia katika mfumo wa vyama vingi tangu talifa hilo lilipopata uhuru wake mwaka 1956.

Moncef Marzouki amekubali kushindwa, na amempongeza mshindi wa uchaguzi wa urais Beji Caïd Essebsi, Adnène Mancer, aliye simamia kampeni ya rais anaye maliza muda wake amesema kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Tume huru ya uchaguzi (ISIE) imekua ikisubiriwa kutangaza Jumatatu Desemba 22 matokeo ya uchaguzi. Matokeo hayo ni ya awali, kwani barua za madai zitapaswa ziliyowasilishwa kwenye tume hiyo kujadiliwa.

Awali chama cha Nidaa Tounes kilitangaza ushindi wa mgombea wake Beji Caid Essebsi, bila kufafanua kura alizopata dhidi ya msindani wake, Moncef Marzouki, rais anaye maliza muda wake.

Vituo vya kupigia kura vilifungwa Jumapili Desemba 21 kwenye saa 12 jioni saa za Tunisia.

Mohsen Marzouk aliye kuwa akisimamia kampeni ya Beji Caid Essebsi, alifanya mkutano na vyombo vya habari akieleza kuwa kulingana na uchunguzi walioendesha kuhusu matokeo ya uchaguzi, mgombea wa chama cha Nidaa Tounes ameshinda uchaguzi.

Marzouk amesema kuwa Caid Essebsi amemshinda kwa kishindo mshindani wake, bila hata hivyo kufafanua kura alizopata.

" Kwa mujibu wa viashiria ambavyo tunavyo, Mheshimiwa Beji Caid Essebsi ni mshindi wa uchaguzi wa rais. Nadhani kuna tofauti kubwa kati ya kura alizopata na alizopata mshindani wake. Tunamshukuru mshindani wetu bila shaka, mgombea Moncef Marzouki, kwa sababu ili kuwepo na demokrasia halisi ni lazima kuwepo na [wagombea] wawili", amesema Marzouk.

Mohsen Marzouk tayari ametangaza kuanza kazi hivi karibuni, huku akitoa kipaumbele kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Marzouk amewatolea wito wafuasi wa Beji Caid Essebsi kuelewa matokeo haya. Amewatolea wito pia kudumisha umoja wa kitaifa na kuahidi kushirikiana na wanasiasa wote ili kuendeleza gurudumu la siasa nchini Tunisia.

" Kila mtu anapaswa kuelewa kuwa ni lazima kuchukua matokeo haya kwa staha kubwa kwa sababu kibarua kinachotusubiri katika sekta ya maendeleo, uchumi na jamii ni muhimu sana'', amesema Marzouk.

Mpaka sasa matokeo rasmi hayajatangazwa, lakini baada ya tangazo lililotolewa na chama cha Nidaa Tounes, bendera za chama cha Nidaa Tounes zimewekwa hewani kwenye milingoti pamoja na picha ya Beji Caid Essebsi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.