Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-SERIKALI-UTEUZI-Siasa

Serikali mpya yatangazwa Madagascar

Siku kumi baada ya uteuzi wa Jean Ravelonarivo kwenye wadhifa wa Waziri mkuu wa madagascar, orodha ya wajumbe wapya wa watakaounda baraza la mawaziri imekabidhiwa Ikulu ya Iavoloha Jumapili Januari 26.

Waziri mkuu Jean Ravelonarivo (kushoto) na mtangulizi wake Kolo Roger (kulia).
Waziri mkuu Jean Ravelonarivo (kushoto) na mtangulizi wake Kolo Roger (kulia). Présidence malgache / Service de presse
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri thelathini na katibu dola mmoja wakiwemo wale walihudumu katika serikali ya zamani wameteuliwa. Kolo Roger, aliyekuwa Waziri mkuu wa zamani na Waziri wa afya ameondolea kwenye orodha hiyo.

Mawaziri wanane ni wapya katika serikali hiyo inayoongozwa na Jean Ravelonarivo, huku 22 wakiwa ni mawaziri waliokua wakihudumu katika serikali ya zamani licha ya kuwa baadhi yao walibadilishiwa wizara.

Béatrice Attalah, ambae alikua mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi nchini Madagascar, ameteuliwa kuwa Waziri wa mambo ya nje. Mshirika wa karibu na msaidizi wa zamani wa rais Hery Rajaonarimampianina, Béatrice Attalah alituhumiwa kujipendelea kwa kutia mbele uchaguzi wake kwenye kiti cha urais.

Uteuzi huu wa Béatrice Attalah, mwaka mmoja baada ya uchaguzi huenda ukaibua maswali mengi kuhusu uadilifu wake pamoja na mchakato wa uchaguzi.

Onitiana Realy, mwanahabari katika masuala ya siasa, ambae ni mashuhuri kwa uzungumzaji wake na uandaaji wa vipindi vyake vya siasa katika redio moja ya kibinafsi nchini Madagasca, ni miongoni mwa Mawaziri hao wapya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.