Pata taarifa kuu
MAREKANI-LIBYA-IS-USALAMA

Afisaa anayehusika na kusajili wapiganaji katika IS auawa

Afisaa anayehusika na kusajili wapiganaji katika kundi la Islamic State ameuawa na mashambulizi ya angani ya ndege za Marekani katika mji wa Mosul nchini Iraq, Juni 15 mwaka 2015. Taarifa hii imetangazwa Jumatatu jioni wiki hii na uongozi wa jeshi la Marekani, Pentagon.

Ndege mbili za kivita za MArekani F/A-18E Super Hornet, zikiwa tayari kwa kuruka ili kushiriki katika mashambulizi dhidi ya Islamic State, tarehe 23 Septemba mwaka 2014.
Ndege mbili za kivita za MArekani F/A-18E Super Hornet, zikiwa tayari kwa kuruka ili kushiriki katika mashambulizi dhidi ya Islamic State, tarehe 23 Septemba mwaka 2014. REUTERS/U.S. Navy
Matangazo ya kibiashara

Ali Awni Al-Harzi alikua akitafutwa na Marekani tangu shambulio dhidi ya ubalozi mdogo wa Marekani katika mji wa Benghazi Septemba mwaka 2012.

Ali Awni Al-Harzi ameuawa katika mashambulizi ya angani yaliyoendeshwa katika mji wa Mosul, mji wa Iraq uliyoanguka mikononi mwa magaidi wa kundi la Islamic State mwaka mmoja uliyopita. Katika taarifa fupi, Pentagon imetangaza kifo cha mwanajihadi huyo aliyekua akitafutwa kwa udi na uvumba na Marekani.

Ali Awni Al-Harzi anatuhumiwa kushiriki katika shambulio dhidi ya ubalozi mdogo wa Marekani katika mji wa Benghaz, nchini Libya mwezi Septemba mwaka 2012. Shambulio ambalo liliwaua wanadiplomasia wanne, ikiwa ni pamoja na balozi Christopher Stevens.

Ali Awni Al-Harzi ambaye alikua akisafiri kwa kutumia pasipoti za uongo, alikamatwa Uturuki na baadaye alirudishwa nyumbani, nchini Tunisia. Alihojiwa kwa muda mfupi na Idara ya ujasusi ya Marekani, na aliachiliwa huru na viongozi wa Tunisia.

Ali Awni al-Harzi pia anatuhumiwa kusafirisha wapiganaji wa kigeni kwa kujiunga na kundi la Islamic State.

“ Ni pigo kubwa kwa kundi la Islamic State. Ni moja ya madaraja ya kundi hilo kwa kusajili na kuwasafirisha wapiganaji wapya nchini Syria na Iraq mbalo limevunjika”, Pentagon imeandika, huku ikibaini kwamba Ali Awni al-Harzi anatuhumiwa pia kupanga mashambulizi mengi ya kujitoa mhanga.

Nduguye Tareq anatafutwa pia na Marekani. Marekani imetenga kitita cha dola milioni 3 kwa taarifa yoyote itakayopelekea kukamatwa kwa Tareq.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.