Pata taarifa kuu
MAREKANI-MKUTANO-UGAIDI-USALAMA

Vita dhidi ya ugaidi: mkutano wa kimataifa wa siku 3 Washington

Viongozi kutoka nchi sitini wanakutana kwa muda wa siku tatu mjini Washington, nchini Marekani, tangu Jumatano wiki hii hadi Ijumaa Februari 20.

Rais wa Marekani Barack Obama aliomba Baraza la Wawakilishi Jumatano Februari 11 kumruhusu rasmi kutumia nguvu dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu. Hapa, ni katika mkutano wa waandishi wa habari katika Ikulu ya White House tarehe 9 Februari mw
Rais wa Marekani Barack Obama aliomba Baraza la Wawakilishi Jumatano Februari 11 kumruhusu rasmi kutumia nguvu dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu. Hapa, ni katika mkutano wa waandishi wa habari katika Ikulu ya White House tarehe 9 Februari mw REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wamewakilisha nchi zao ambazo zilialikwa na Marekani kwa lengo la kujadili jinsi gani makundi ya kigaidi, hususan kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu, Al Qaeda, Boko Haram, Al Shabab, na mengineyo ambayo yanajihusisha na ugaidi yanaweza kutokomezwa

Kwa mujibu wa mwanahabari wa RFI, mjini Washington, Guilhem Delteil, baadhi ya nchi zimewatuma mawaziri wao wa mambo ya nje. Misri ambayo iliendesha mashambulizi Jumanne wiki hii dhidi ya ngome za kundi la wanamgambo wa kiislamu lenye uhusiano na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu nchini Libya, ambalo liliwakata vichwa Wakristo 21 wa madhehebu ya Coptic kutoka Misri, imewakilishwa katika mkutano huo na Waziri wake wa mambo ya nje.

Viongozi hao wanatazamiwa pia kujadili masuala ya kijeshi katika vita dhidi ya ugaidi. Lakini si suala hilo pekee litakalojadiliwa katika mkutano huo. Mataifa mengine kama, Ufaransa, yatawakiliswa na mawaziri wao wa mambo ya ndani. Marekani inataka mbinu ya pamoja ya kutokomeza ugaidi duniani.

Moja ya mada kuu ya majadiliano itakuwa kuzuia itikadi kali za kidini ili kuepuka kuimarisha makundi haya, lakini pia kupunguza tishio la kigaidi duniani.

Mashambulizi karibu yote yaliyotokea Canada mwezi Oktoba mwaka jana, Australia mwezi Desemba mwaka jana, Ufaransa mwezi Januari mwaka huu au Denmark mwishoni mwa juma llilopita, yaliendeshwa kwa itikadi kali za kidini kupitia baadhi ya raia 3000 kutoka nchi za Magharibi ambao walijiunga na makundi ya wanajihadi nchini Syria na Iraq.

Hali hii ya wapiganaji wa kigeni wanaojiunga na makundi ya wanajihadi inawatia hofu viongozi wa nchi za Kiarabu. Raia wa Jordan na Tunisia ni wengi zaidi nchini Syria.

Mara nyingi raia hao wanajiunga na makundi haya ya kigaidi kutokana na ukosefu wa ajira, ubaguzi katika kijamii pamoja na ukosefu wa uwakilishi wa kisiasa. Sababu ni nyingi zinazopelekea hali hii kuendelea kukua, na sababu hizo ndizo zinatazamiwa kujadiliwa kwa pamoja katika mkutano wa kilele unaoanza Jumatatu wiki hii mjini Washington, Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.