Pata taarifa kuu

Marekani: Takriban watano wafariki baada ya vimbunga kupiga Oklahoma

Takriban watu watano wamepoteza maisha baada ya baadhi ya vimbunga vingi kupiga sehemu ya Mabonde Makuu ya katikati mwa Marekani, viongozi wa eneo hilo wamesema siku ya Jumapili usiku Aprili 28. Baada ya vimbunga 78 kurekodiwa siku ya Ijumaa, haswa huko Iowa na Nebraska, vingine 35 vilirekodiwa Jumamosi kutoka kaskazini mwa Texas hadi Missouri, kulingana na mamlaka ya hali ya hewa nchini Marekani (NWS), linaandika shirika la habari la AFP.

Huku watu 228 wakiwa wamefariki, 1,700 kujeruhiwa na watu milioni moja bila umeme, Alabama ndilo jimbo lililoathiriwa zaidi na kimbunga katika siku za hivi karibuni nchini Marekani.
Huku watu 228 wakiwa wamefariki, 1,700 kujeruhiwa na watu milioni moja bila umeme, Alabama ndilo jimbo lililoathiriwa zaidi na kimbunga katika siku za hivi karibuni nchini Marekani. REUTERS/Marvin Gentry
Matangazo ya kibiashara

Gavana wa Oklahoma Kevin Stitt amethibitisha siku ya Jumapili usiku vifo vya watu wanne katika jimbo hilo. Mwanamke mmoja alifariki katika mji mdogo wa Sulphur, ambao uliathirika zaidi, alisema katika mkutano na waandishi wa habari. Picha na video zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha makumi ya nyumba zimeharibiwa kabisa na magari yameharibiwa vibaya.

Zaidi ya kilomita 100 kutoka, huko Holdenville, angalau watu wengine wawili walipoteza maisha, kulingana na idara ya usimamizi wa majanga, na vyombo vya habari vya ndani vikiripoti mtoto mchanga wa miezi minne kati ya waathirika. Shughuli za usafishaji ziliendelea Jumapili.

Mtu wa nne alifariki kwenye barabara kuu huko Marietta, katika jimbo hilo. 

Hali ya hatari Oklahoma

Gavana wa Oklahoma ametangaza hali ya hatari kwa siku thelathini. Mvua kubwa pia imerekodiwa katika maeneo kadhaa na tahadhari za hali ya hewa ziliendelea kutumika siku ya Jumapili, ikiwa ni pamoja na hatari ya mafuriko, mvua ya mawe na vimbunga.

Huko Iowa, mwathiriwa wa tano, mwanamume, alifariki kutokana na majeraha hospitalini, familia yake imekiambia kituo cha habari cha KETV NewsWatch 7.

Zaidi ya nyumba 2,000 hazikuwa na umeme huko Texas na zaidi ya 19,000 huko Oklahoma kufikia Jumapili alasiri, kulingana na tovuti ya PowerOutage.

Vimbunga, matukio ya hali ya hewa ya kutisha ambavyo ni vigumu kutabiri, hutokea mara kwa mara nchini Marekani, hasa katikati na kusini mwa nchi. Hata hivyo, ni nadra sana kwa vimbunga vikubwa kupishana kwa muda mchache, kulingana na wataalamu wa hali ya hewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.