Pata taarifa kuu
UHALIFU-USALAMA

Ecuador: Kiongozi wa genge la Lobos akamatwa

Ingawa walikataa mapendekezo ya kiuchumi ya Rais Daniel Noboa wakati wa kura ya maoni ya Jumapili, wananchi wa Ecuador kwa kiasi kikubwa waliunga mkono vita vyake dhidi ya uhalifu na ulanguzi wa dawa za kulevya. Katika muktadha huu, kukamatwa kwa mmoja wa wahalifu wanaosakwa sana nchini kunakuja wakati mwafaka kwa serikali.

Ecuador: kiongozi wa genge la Lobos, Kapteni Pico, alikamatwa na wanachama kadhaa wa kundi la wasaidizi wake Jumatatu usiku. Anashukiwa kuwa chanzo cha mauaji ya Fernando Villavicencio, mgombea urais mwezi Agosti mwaka jana.
Ecuador: kiongozi wa genge la Lobos, Kapteni Pico, alikamatwa na wanachama kadhaa wa kundi la wasaidizi wake Jumatatu usiku. Anashukiwa kuwa chanzo cha mauaji ya Fernando Villavicencio, mgombea urais mwezi Agosti mwaka jana. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Fabricio Colón Pico, almaarufu Kapteni Pico, ni mmoja wa viongozi wakuu wa genge la Lobos, Wolves, mojawapo ya magenge yenye nguvu na vurugu nchini Ecuador. Alitoroka Januari 9 kutoka gereza la Riobamba, wakati wa machafuko yaliyofuatia kutangazwa kwa hali ya hatari. Familia yake ilikuwa imetangaza kifo chake lakini baada ya uchunguzi wa miezi kadhaa, Fabricio Colón alipatikana kwenye hacienda (shamba) ya kakao yenye ukubwa wa hekta 22 katika mji mdogo wa Puerto Quito, kaskazini magharibi mwa mji mkuu.

Licha ya kuwepo kwa walinzi wengi, polisi walifanikiwa kuzingira hacienda saa tatu asubuhi Jumatatu kabla ya kushambulia. Baada ya kupigwa risasi, Fabricio Colón alikamatwa akiwa na washirika wake akiwemo dadake wakiwa na silaha, pesa na simu 7, anaripoti mwandishi wetu wa Quito, Eric Samson. Kapteni Pico, ambaye alipaka nywele zake rangi ya kimanjano na kubadilisha sura yake, alikuwa mmoja wa watu waliotafutwa sana nchini.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Monica Palencia, alipendekeza kuwa kiongozi wa Lobos aligunduliwa alikojificha kupitia namba ya simu kwa 131, nambari maalum iliyowekwa na mamlaka ili kkupokea habari kwa ambaye atafichua aliko kiongozi huyo na kweza kupewa zawadi. "Watu walizungumza nasi kwa uwazi na kwa ufupi, na kutuambia kwamba kipaumbele chao kilikuwa usalama, na tunalifanyia kazi," amesema Bi. Palencia, akizungumzia kura ya maoni ya Jumapili ambayo iliidhinisha mapendekezo tisa kutoka kwa Rais Noboa ya kupambana na uhalifu. Serikali inatarajia kuwasili bungeni rasimu hii inayolenga kurekebisha Katiba na Kanuni ya Adhabu ili kutekeleza hatua zilizoidhinishwa kama vile kuwarejesha wahalifu nchini.

Mamlaka inashuku Los Lobos kwa kuhusika katika mauaji ya mgombea urais Fernando Villavicencio, aliyepigwa risasi na wapiganaji wa Colombia akitoka kwenye mkutano wa kampeni huko Quito mwezi Agosti mwaka jana. Mlengwa mwingine wa genge hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Diana Salazar, ambaye anaongoza mapambano ya kisheria dhidi ya makundi ya uhalifu na uchunguzi kadhaa ambao umefichua uhusiano wao na wanasiasa, majaji na maafisa wakuu. Anachukuliwa kuwa mmoja wa watu wanaofanyiwa vitisho vikubwa nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.