Mexico yasitisha uhusiano wake kidiplomasia na Ecuador
Nairobi – Mexico imetangaza kusitisha uhusiano wake wa kidiplomasia na nchi ya Ecuador baada ya polisi kuvamia ubalozi wa Mexico mjini Quito wakiwa na lengo la kumkamata makamu wa Rais wa zamani wa Ecuador Jorge Glas.
Imechapishwa:
Glas alitorokea katika ubalozi huo mwezi Desemba mwaka wa 2023 baada ya Ecuador kutoa hati ya kukamatwa kwake akidaiwa kuhusika na ufisadi.
Kwa mujibu wa wakili wa Glas aliyehudumu katika wadhifa wa makamu wa rais wa Ecuador kati ya 2013 na 2017, kiongozi huyo wa zamani hana hatia.
Makamu huyo wa rais wa zamani aliondolewa katika wadhifa wake kutokana na madai ya kujihusisha na ufisadi akiwa afisa wa umma.
Alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela baada ya kuondolewa afisini kwa kuhusishwa na ufisadi katika kampuni kubwa ya ujenzi ya Brazil Odebrecht.
Kwa mujibu wa taarifa ya waendesha mashtaka, kiongozi huyo wa zamani alipokea Dolla Milioni 13.5 kama hongo.
Aliachiwa kutoka gerezani Novemba mwaka jana lakini mamlaka ya Ecuador ikatoa hati nyingine ya kukamatwa kwa tuhuma zaidi ya rushwa, hali iliompekea kutafuta kumfanya hifadhi katika ubalozi wa Mexico.
Mexico ilisema ilitoa kibali kwa Glas kuishi nchini humo baada ya kuchunguza kwa udani hali aliokuwa anakabiliwa nayo.
Hatua hii inakuja baada ya siku ya Ijumaa, mamlaka nchini Morocco kulalamikia kile ilichosema ni unyanyasaji kutokana na uwepo wa maofisa wa polisi katika ubalozi wake wa Quito.