Pata taarifa kuu

Marekani: Trump ametuhumiwa kwa njama ya uhalifu wa kuficha ukweli

Viongozi wa mashtaka nchini Marekani, wamemtuhumu rais wa zamani, Donald Trump kwa kuhusika kwa njama ya uhalifu na kuficha ukweli, katika kesi dhidi yake iloanza kuskilizwa Jumatatu ya wiki hii.

Rais wa zamani wa Marekani na mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump akiwa mahakamani katika siku ya kwanza ya ufunguzi wa kesi yake katika Mahakama ya Jinai ya Manhattan mjini New York, Marekani, Aprili 22, 2024.
Rais wa zamani wa Marekani na mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump akiwa mahakamani katika siku ya kwanza ya ufunguzi wa kesi yake katika Mahakama ya Jinai ya Manhattan mjini New York, Marekani, Aprili 22, 2024. © Victor J. Blue / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Keshi hii ya uhalifu dhidi ya Donald Trump, ni ya kwanza kufunguliwa dhidi ya aliyekuwa rais wa Marekani.

Kiongozi wa mashtaka Matthew Colangelo amesema Donald Trump alitoa taarifa za uongo za kibiashara na kumlipa muigizaji wa filamu za ngono Stormy Daniels, ili kumzuia kutoa taarifa ambazo zingekuwa na athari kubwa katika maisha yake ya kisiasa mwaka 2016, alipowania urais kwa mara ya kwanza.

Former President Donald Trump, right, speaks to reporters with attorney Todd Blanche at the end of the day at Manhattan criminal court as jury selection continues for Trump's trial in New York, on Thu
Donald Trump ameendelea kusisitiza kuwa kesi dhidi yake imechochewa kisiasa na wapinzani wake. AP - Jabin Botsford

Hata hivyo rais huyo wa zamani wa Marekani, amekanusha madai dhidi yake akisema kesi hiyo inalenga kumchelewesha kundeleza kampeni zake za kuelekea ikulu ya White House Mwezi Novemba.

Trump mwenye umri wa miaka 77 ni rais wa kwanza wa zamani wa Marekani kufunguliwa mashtaka ya uhalifu, na kesi hii inaweza kuwa na athari kubwa kuelekea uchaguzi wa mwezi Novemba ambapo atagombea dhidi ya rais Joe Biden.

Rais Joe Biden anatarajiwa kupambana dhidi ya rais wa zamani Donald Trump katika uchaguzi mkuu wa urais.
Rais Joe Biden anatarajiwa kupambana dhidi ya rais wa zamani Donald Trump katika uchaguzi mkuu wa urais. AP

Katika kesi hii iwapo Trump, atapatikana na hatia basi anaweza kufungwa jela, kutumikia kifungo cha nyumbani au kulipa faini.

Na Benson Wakoli- Rfi-Kiswahili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.