Pata taarifa kuu

Haiti: Baraza tawala la mpito laundwa rasmi

Baraza tawala la mpito nchini Haiti lililokuwa likitarajiwa, hatimaye  limeundwa rasmi, mwezi mmoja baada ya tangazo la kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Ariel Henry.

Ikulu ya rais huko Port-au-Prince, Jumatatu Machi 25, 2024.
Ikulu ya rais huko Port-au-Prince, Jumatatu Machi 25, 2024. AP - Odelyn Joseph
Matangazo ya kibiashara

Baraza tawala la mpito limeundwa, baada ya wiki kadhaa za mazungumzo magumu. Kuundwa kwa chombo hiki kitakachojaribu kurejesha utulivu nchini Haiti, inayokabiliwa na vurugu za magenge yenye silaha, kulifanywa rasmi na agizo lililotiwa saini na Ariel Henry na kuchapishwa katika gazeti rasmi la Le Moniteur. "Majukumu ya Baraza tawala la mpito yanaisha, Februari 7, 2026," kulingana na agizo hilo. Baraza halitaongezewa muda, bada ya muda wake rasmi kukamilika.

Wajumbe wake watalazimika "haraka" kuteua Waziri Mkuu, pamoja na serikali "jumuishi".

Kuhusu uteuzi wa wajumbe tisa wa chombo hiki cha mpito, itabidi kusubiri kwa muda mrefu zaidi, anaripoti mwandishi wetu huko Port-au-Prince, Marie-André Belange. Sheria hiyo, katika Ibara ya 2, inaeleza kwamba hakuna mtu anayeweza kuwa sehemu ya Baraza ikiwa kwa sasa anakabiliwa na mashitaka au amefunguliwa mashtaka ya jinai, au ikiwa amehukumiwa katika mahakama yoyote nchini; ikiwa anakabiliwa na vikwazo vya Umoja wa Mataifa; iwapo atakuwa mgombea katika uchaguzi ujao nchini Haiti au anapinga azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaloidhinisha kutumwa kwa Ujumbe wa Kimataifa wa kusimamia usalama na mamani nchini Haiti.

Kufuatia kuchapishwa kwa sheria hiyo, serikali inayomaliza muda wake, katika barua, iliwataka watu walioteuliwa kuwa sehemu ya Baraza kuwasilisha kwa Sekretarieti Kuu ya Baraza la Mawaziri hati zinazohitajika kwa mujibu wa Ibara ya 2 ya waraka huo. Hata hivyo, Ibara husika hakikutaja nyaraka, bali masharti.

Baraza tawala la Mpito litaendesha vikao vyake katika ikulu ya rais, kulingana na sheria hiyo. Huku eneo ambalo ikulu hiyo inapatikana ni eneo ambalo limekuwa likilengwa na mashambulizi ya majambazi wenye silaha katika wiki za hivi karibuni.

Baraza hilo bado halijasimamia rasmi nchi, na Ariel Henry "atawasilisha kujiuzulu kwa serikali yake kufuatia uteuzi wa Waziri Mkuu mpya", unabainisha waraka huo.

Nchi ya Caribbean imekumbwa na ukosefu wa utulivu wa kisiasa kwa miongo kadhaa. Lakini mwishoni mwa mwezi wa Februari, magenge hayo, ambayo tayari ghasia zao zilikuwa zimeharibu sehemu zote za eneo hilo, yalianzisha mashambulizi yaliyoratibiwa dhidi ya maeneo ya kimkakati, yakisema yanataka kumpindua Waziri Mkuu, Ariel Henry.

Ariel Henry, aliyeteuliwa siku chache kabla ya mauaji ya rais Jovenel Moïse, mwaka 2021, alipingwa vikali. Hakuweza kurejea nchini mwake baada ya ziara yake nchini Kenya. Mnamo Machi 11, siku iliyoendana na mkutano kati ya Wahaiti na mashirika kadhaa na nchi kama vile Marekani, alitangaza kwamba anajiuzulu ili kutoa nafasi kwa baraza hili tawala la mpito.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.