Pata taarifa kuu
LIBYA-WAHAMIAJI-ULAYA-USALAMA

Libya: boti lazama na mamia ya wahamiaji

Boti la uvuvi lililokua limebebea mamia ya wahamiaji limezama Jumatano wi hii, kwenye umbali wa kilomita 30 kutoka pwani ya Libya. Mamia kadhaa ya watu bado hawajulikani walipo.

Wahamiaji kadhaa waliokolewa baada ya kuzama kwa boti yao katika pwani ya Libya, Agosti 5mwa 2015.
Wahamiaji kadhaa waliokolewa baada ya kuzama kwa boti yao katika pwani ya Libya, Agosti 5mwa 2015. REUTERS/Marta Soszynska/MSF
Matangazo ya kibiashara

Shughuli za uokoaji bado zinaendelea. Ajali hii inaweza kuwa kubwa zaidi baada ya ile iliowaua watu 800 mwezi Aprili mwaka huu. Shirika la Kimataifa la Uhamiaji limetangaza kuwa wahamiaji zaidi ya 2,000 wamefariki dunia tangu mwanzoni mwa mwaka huu katika bahari ya Mediterranean.

Watu mia sita ndio walikuwa katika boti hilo la uvuvi lililozama, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR). Watu mia mbili na hamsini waliokolewa na sita walikutwa wamekufa, kwa mujibu wa tathmini ya awali.

Boti hilo liliomba msaada kwa walinzi wa pwani ya Catania, katika jimbo la Sisilia Jumatano asubuhi wiki hii. Meli mbili, moja ya shirika la madaktari wasio na mipaka (MSF) na nyingine ya jeshi la wanamaji la Ireland, ambazo zilikua zilikua zikipiga doria katika eneo hilo, zilitumwa kwenye eneo la tukio.

Kwa mujibu wa msemaji wa UNHCR, boti hilo lilizama kwa haraka kwa sababu lilikuwa la chuma na wahamiaji wengi walinaswa katika boti. Shughuli za uokoaji bado zinaendelea. Meli tano kwa sasa zinaendelea na zoezi la uokoaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.