Pata taarifa kuu
BURUNDI-SHAMBULIO-USALAMA

Burundi: mkuu wa majeshi jenerali Prime Niyongabo aponea kuuawa

Mkuu wa Majeshi ya Burundi Meja jenerali Prime Niyongabo ameponea kuuawa katika shambulio la roketi liliyolenga gari lake. Inaarifiwa kuwa watu waliokua wamevalia sare ya jeshi wameshambulia gari la mkuu wa majeshi ya Burundi karibu na daraja la Muha wilayani Kinindo.

Meja jenerali Prime Niyongabo, Mkuu wa majeshi ya Burundi ameponea kuuawa katika shambilo lililoendeshwa dhidi ya gari lake leo Ijumaaa asubuhi Spemba 11 wakati ambapo alikua akijielekeza kazini.
Meja jenerali Prime Niyongabo, Mkuu wa majeshi ya Burundi ameponea kuuawa katika shambilo lililoendeshwa dhidi ya gari lake leo Ijumaaa asubuhi Spemba 11 wakati ambapo alikua akijielekeza kazini. RFI-KISWAHILI
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limetokea leo Ijumaa saa 12:45 (saa za Afrika ya Kati). Inaarifawa pia kuwa wanajeshi kadhaa wameuawa katika shambulio hilo.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Mkuuwa majeshi ya Burundi, Meja Jenerali Prime Niyongabo hakupata jeraha lolote katika shambulio hilo lililoendeshwa na kundi ambalo hadi sasa bado halijajulikana karibu na daraja la Muha, kwenye barabara inayoelekea mkoani Rumonge kusini mwa Burundi.

Kwa mujibu wa mashahidi, kumesikika milio mingi ya milio ya risasi na milipuko ya mabomu. " Nimeona gari ndogo la kijeshi likishambuliwa kwa risasi. Nimeona pia miili ya wanajeshi 2 au 3 ikiwa katikati ya barabara ", amesema shahidi mmoja wa mashahidi hao. Gari dogo lingine la polisi limerushiwa risasi karibu na Hospitali ya Kira , karibu na eneo la shambulizi. Inakisiwa kuwa askari polisi kadhaa wamejeruhiwa katika shambulio hilo dhidi ya gari lao.

Barabara hiyo inayoelekea mkoani Rumonge imefungwa kwa muda wa zaidi ya saa moja, madereva wa magari ambayo walikuwa wakisafiri kwenda mjini kati Bujumbura waliamua kutumia barabara nyingine. Wanajeshi wengi wakiwa na silaha za kivita wamwekwa tangu baada ya jaribio la mapinduzi lililotibuka mwezi Mei kwenye barabara hiyo inayotumia kila mara asubuhi na Mkuu wa majeshi ya Burundi anapojielekeza kazini.

Hali ya usalama nchini Burundi, hasa katika mji wa Bujumbura imeendelea kuzorota, baada tu ya rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kamua kuwania muhula wa pili, ambao ni kinyume na Katiba na Mkataba wa amani na maridhaiano wa Arusha, kwa mujibu wa upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.