Pata taarifa kuu
UGANDA-DRC-ADF-USALAMA

Uganda / DRC: uwezekano wa uwepo wa waasi wa ADF mpakani

Mashariki mwa DRC katika wiki za hivi karibuni kulishuhudiwa ongezeko la machafuko ya kundi la waasi wa ADF. Kundi hili la waasi kutoka Uganda lilifurushwa rasmi katika ardhi ya Uganda. Hata hivyo kuna uvumi kwamba bado kundi hilo linaendesha harakati zake nchini Uganda.

Gari la jeshi la Uganda limeegeshwa karibu na milima wa Rwenzori, si mbali na kijiji cha Kichwamba (kusini magharibi mwa Uganda), skaribu na mpaka wa DRC, Desemba 2015.
Gari la jeshi la Uganda limeegeshwa karibu na milima wa Rwenzori, si mbali na kijiji cha Kichwamba (kusini magharibi mwa Uganda), skaribu na mpaka wa DRC, Desemba 2015. © Gaël Grilhot/RF
Matangazo ya kibiashara

Mjini Kampala, hawana shaka kwamba waasi wa ADF wanaendesha harakati zao nje ya Uganda. Lakini wamekua wakijaribu kuvuka mpaka na kuendesha machafuko nchini humo. Hayo yamefahamishwa na Waziri wa ulinzi wa Uganda Krispo Kiyonga."Tunawasubiri mpakani iwapo wanakuja, wao ndio watakufa, si raia wetu . "

Lakini karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hali inaonekana kuwa tete. Ni vigumu kudhibiti hali ya mambo katika eneo la Mpondwe. Katika milima ya Rwenzori, wafanyabiashara wanakabiliwa na visa vya uporaji, utekaji nyara na mauaji. Luteni Nsamba anakubali kwamba si rahisi kudhibiti hali ya usalama kwenye mpaka.

"Nataka kuwaonyesha jinsi kudhibiti mipaka barani Afrika ni vigumu ikilinganishwa kwa mfano na mipaka ya Ukraine au Ubelgiji. Katika nchi hizo, wakati kunaonekana tatizo la wakimbizi, kwa mfano, nchi hizi zinaharakia moja kwa moja kuweka vizuizi. Kwa hiyo mipaka na usimamizi kwenye mipaka hiyo vinakwenda sambamba na teknolojia", amesema Kanali Nsamba.

Hata hivyo wakazi wa kijiji cha Kichwamba nchini Uganda, wanasema wanatiwa hofu na hali ya usalama ambayo inaendelea kudorora siku baada ya siku. Mkazi mmoja wa kijiji hicho amesema kuna uvumi kwamba waasi wa ADF bado wapo nchini Uganda. "Ni rahisi. Wanaweza kujifananisha na raia wa kawaida. Si rahisi kuwatambua."

Kirasmi, waasi wa ADF wako upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Vyombo vya habari nchini Congo vimearifu kwamba waasi hao walionekana hivi karibuni upande wa Ntoroko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.