Pata taarifa kuu
ICC-AFRIKA KUSINI-HAKI

ICC:Afrika Kusini ilishindwa kutekeleza wajibu wake

Mahakama ya Kimataifa ya ICC, imesema kuwa Afrika Kusini ilikuwa na jukumu la kumkamata rais wa Sudan Omar al-Bashir aliezuru nchi hiyo mwaka 2015.

Rais wa sudan, Omar Al Bashir, akiwasili Khartoum, Juni 15 mwaka 2015, akitokea Johannesburg.
Rais wa sudan, Omar Al Bashir, akiwasili Khartoum, Juni 15 mwaka 2015, akitokea Johannesburg. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

ICC imepuuzilia mbali utetezi wa Afrika Kusini kuwa nchi hiyo ilikuwa na kinga ya kutomkamata rais Bashir anayetafutwa kwa madai ya kutekeleza mauaji ya maelfu ya watu katika jimbo la Darfur. Hata hivyo, Mahakama hiyo haijairipoti Afrika Kusini katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mawakili na wachambuzi wa Mambo wanasema kuwa walitarajia kuipata na hatia taifa la Afrika Kusini kushindwa kutekeleza jukumu lake kama mwachama wa Mahakama hiyo.

ICC inaamini kwamba Pretoria imeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kimataifa wakati ilishindwa kumkamata rais wa Sudan wakati ambapo alikua katika ardhi yake. Wakati wa kusoma uamuzi huo, jaji alikumbusha kwamba miezi miwili kabla ya Omar al-Bashir kuelekea Afrika Kusini katika mkutano wa Umoja wa Afrika, Mahakama ya Pretoria iliwasiliana na serikali ya Pretoria na kuomba kushirikiana.

Mahakama ilikumbusha kwamba Afrika Kusini, kama nchi yoyote wanachama ana wajibu wa kumzuia mtu anaetafutwa na ICC. Na ilibainisha kuwa Afrika Kusini haiwezi kuzungumzia kinga yoyote kwa anaeshtumiwa uhalifu wa kivita. Hakuna mgogoro au utata, alihitimisha jaji Cuno Tarfusser, huku akibaini kwamba Afrika Kusini imeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kimataifa na kuaathiri kazi ya Mahakama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.