Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SUDANI-MSRI-NILE-USHIRIKIANO

Mazungumzo kuhusu matumizi ya Mto Nile yaambulia patupu

Mazungumzo ya hivi karibuni kupata mwafaka kuhusu mzozo wa matumizi ya maji ya mto Nile kuzalisha umeme kwenye mradi mkubwa nchini Ethiopia yamekamilika bila ya pande zote zinazotofautiana kukubaliana

Bwawa kubwa la Grande Renaissance lililojengwa nchini Ethiopia katika mkoa wa Benishangul Gumuz, kwenye Mto Blue Nile. picha iliyopigwa Machi 2015.
Bwawa kubwa la Grande Renaissance lililojengwa nchini Ethiopia katika mkoa wa Benishangul Gumuz, kwenye Mto Blue Nile. picha iliyopigwa Machi 2015. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo ya hivi punde yalioongozwa na rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.

Ajenda kubwa ilikuwa ni kufahamu iwapo mpango wa Ethiopia kujaza bwawa hilo kwa kutumia maji ya Mto Nile, hautaathiri upatikanaji wa maji kwa nchi za Misri na Sudan.

Hata hivyo, baada ya misururu ya mazungumzo, Aaziri wa Maji wa Ethiopia, Seleshi Bekele, amesema hakuna makubaliano yaliyofikiwa na kuishtumu Misri na Sudan kuwasilisha masharti mapya.

Mataifa hayo matatu yamekuwa yakizozana kuhusu ujenzi wa bwawa hilo kubwa barani Afrika, Ethiopia ikiendelea kusisitiza itaendelea na mpango wake wa kutumia maji hayo, lakini Misri inasema mradi huo utafanya nchi hiyo kukosa maji kwa sababu Mto Nile ndio chanzo chake kikubwa.

Juhudi za kujaribu kupata  mwafaka kuhusu mzozo huu chini ya usluhishi wa Marekani pia haujafua dafu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.