Pata taarifa kuu
MSUMBIJI

Msumbiji: Maelfu ya raia wakimbia vurugu za wanajihadi

Maelfu ya watu wamekuwa bado wakijaribu kwa njia zote kuyatoroka makaazi yao, Kaskazini Mashariki mwa Msumbiji, inayokabiliwa na mashambulizi makubwa ya wanajihadi tangu Jumatano ambayo yameua raia wengi.

Mji wa Cabo Delgado umeendelea kukumbwa na mapigano kati ya vikosi vya serikali ya Msumbiji na wanajihadi..
Mji wa Cabo Delgado umeendelea kukumbwa na mapigano kati ya vikosi vya serikali ya Msumbiji na wanajihadi.. © RFI/Amnesty International
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili jioni Serikali ya Msumbiji ilithibitisha kwamba watu wasiopungua saba waliuawa katika shambulio la Ijumaa, wakijaribu kutoroka kutoka hoteli walikokuwa wamekimbilia.

Na wengi "kadhaa" waliuawa katika shambulio la kwanza siku ya Jumatano dhidi ya mji mdogo wa Palma, ulio kilometa kumi tu kutoka eneo la gesi linalosimamiwa na kapmuni ya Ufaransa ya TOTAL, ambayo imeanzisha mradi mkubwa wa dola bilioni ishirini, unaotakiwa kuwa umeanza kutumika mwaka 2024.

Mji wa Palma ulianguka mikononi mwa makundi haya yenye silaha siku ya Ijumaa jioni, baada ya zaidi ya saa 48 ya mapigano.

"Zaidi ya watu mia moja wametoweka," mtafiti Martin Ewi, kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Usalama huko Pretoria, ameliambia shirika la haari la AFP, akibaini kwamba "hali bado ni tete katika mji huo".

Wanajihadi, ambao wametangaza kuungana na kundi la Islamic State, na ambao, kwa zaidi ya miaka mitatu, wameendelea kutishia maisha ya wakaazi wa jimbo lenye Waislamu wengi la Cabo Delgado, linalopakana na Tanzania,  walifanya mashambulizi ya kushtukiza kwa wakati mmoja Jumatano alasiri kutoka eneo la pande tatu, na kusababisha hofu kwa wakaazi wake 75,000. .

Mashahidi waliliambia shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch kwamba walifyatua risasi "kila mahali, wakilenga watu na majengo", na kuacha miili ya watu barabarani.

Wakimbizi watumia boti kwa kuokoa maisha yao

"Vitendo vyao vilisababisha mauaji ya makumi ya watu wasio na ulinzi," Kanali Omar Saranga, msemaji wa Wizara ya Ulinzi, ameshutumu katika mkutano na waandishi wa habari.

Wakazi, pamoja na wakimbizi wengi ambao tayari wametoroka vurugu za wanajihadi katika vijiji vyao, wameanza tena kukimbia.

Wengine wamekimbilia kuelekea misitu ya karibu, wengine kuelekea fukwe wakitumia usafiri wa boti. Wengine waliondoka kwa miguu au kwa magari kwenda kwenye eneo la gesi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.