Pata taarifa kuu
UFARANSA-ULINZI

Mali: Ndege ya kijeshi ya Ufaransa Mirage 2000 yaanguka Hombori

Marubani wawili wa ndege ya kivita ya Ufaransa iliyoharibiwa vibaya walinusurika kifo baada ya ndege yao kuanguka katika eneo la Hombori, kabla ya kupatikana, jeshi limesema Jumanne wiki hii.

Ajali hiyo ilitokea wakati wa ujumbe wa msaada wa anga kwa shirika la Ufaransa la GTD na kikosi cha wanajeshi wa Mali, katika shughuli ya upelelezi kando ya barabara ya kuu ya 16 kuelekea kusini mwa eneo la Hombori.
Ajali hiyo ilitokea wakati wa ujumbe wa msaada wa anga kwa shirika la Ufaransa la GTD na kikosi cha wanajeshi wa Mali, katika shughuli ya upelelezi kando ya barabara ya kuu ya 16 kuelekea kusini mwa eneo la Hombori. © AFP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Mmoja wa marubani, amejeruhiwa kidogo na kupelekwa katika kambi ya kijeshi ya Gao, idara ya vyombo vya habari vya jeshi imesema.

Marubani hao wawili wamepatikana katika eneo ambalo halikaliwi na watu na ndege hiyo pia ilianguka katika eneo lisilokaliwa na watu, kulingana na chanzo hicho. Mabaki ya ndege hiyo yaligunduliwa na kikosi cha Barkhane.

Ajali hiyo ilitokea wakati wa ujumbe wa msaada wa anga kwa shirika la Ufaransa la GTD na kikosi cha wanajeshi wa Mali, katika shughuli ya upelelezi kando ya barabara ya kuu ya 16 kuelekea kusini mwa eneo la Hombori.

Eneo la Hombori, na mkoa wote wa Mopti, ni eneo la operesheni lililolengwa hasa na vikosi vya Barkhane katika miezi ya hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.