Pata taarifa kuu
CAR-HAKI

Jamhuri ya Afrika ya Kati: kiongozi wa anti-balaka Eugène Ngaïkosset akamatwa

Eugène Ngaïkosset, kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Kikristo la Anti-balaka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na afisa wa zamani wa kikosi cha ulinzi wa rais wa zamani wa nchi hiyo François Bozizé, yuko mikononi mwa idara za usalama.

Mazingira ya kukamatwa kwa Eugène Ngaïkosset, mshirika wa karibu wa François Bozizé, bado hayajajulikana
Mazingira ya kukamatwa kwa Eugène Ngaïkosset, mshirika wa karibu wa François Bozizé, bado hayajajulikana © AFP/FLORENT VERGNES
Matangazo ya kibiashara

Habari hiyo imethibitishwa kwa RFI na Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, lakini mazingira ya kukamatwa kwake bado hayajaelezwa. Eugène Ngaïkosset anatuhumiwa kwa vitendo vingi vya uhalifu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Eugène Ngaïkosset, ambaye anatimiza miaka 54 ya kuzaliwa mwaka huu, ni rafiki wa zamani na mshirika wa karibu wa rais wa zamani wa Jamhuri ya afrika ya Kati François Bozizé, ambaye wakati huo alikua na cheo cha Kepteni kwenye kikosi cha ulinzi wa rais.

Aliitwa "mchinjaji wa Paoua" kwa jukumu lake katika operesheni zilizoendeshwa kumaliza uasi ambao ulikuwa ulizuka kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya François Bozizé kuchaguliwa kuwa rais katika uchaguzi wa mwaka 2005. Kwa kipindi cha miaka miwili, kikosi hiki cha ulinzi wa rais kiliua raia mia kadhaa katika jimbo hilo.

Katika kipindi hiki, shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch lilisema askari walifyatua risasi kwenye umati wa watu, wakipora na kuchoma maelfu ya nyumba, wakati mwingine wakiteketeza kwa moto vijiji vyote. Eugène Ngaïkosset alikuwa mkuu wa moja ya vitengo vilivyohusika katika uhalifu huo, kulingana na HRW.

Alikamatwa nchini Congo baada ya kuanguka kwa utawala wa Bozizé, kisha akarudishwa nchini, lakini alitoroka Bangui mnamo mwaka 2015 kabla ya kuchukua silaha.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linamshutumu kuwa mmoja wa wahusika wakuu wa vurugu zilizotokea katika mji mkuu Bangui miezi michache baadaye. "Yeye na wapiganaji wengine wa kundi la Anti-balaka walijiunga na waasi wa zamani wa Seleka ili kuiangusha serikali ya mpito," kulingana na Umoja wa Mataifa. Tangu wakati huo hakurudi kuonekana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.